Njombe
Serikali imewahakikishia manufaa makubwa na kuwaomba subira wananchi wa vijiji vya amani na Mundindi na vile vinavyopakana na miradi mikubwa ya Liganga na Mchuchuma iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe kutokana na wananchi waliokuwa wanamiliki maeneo ya karibu na miradi hiyo kuhamishwa katika maeneo hayo huku wakisubiri fidia kwa muda mrefu mpaka sasa.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Mundindi waziri wa madini Doto Mashaka Biteko amesema serikali haiwezi kuwatupa wananchi wa kata na vijiji jirani na miradi hiyo kwa kuwa licha ya kusimama kwa muda mrefu lakini serikali imefikia hatua nzuri ya makubaliano baina ya serikali na wawekezaji.
"Wale wananchi wenye mashamba yao na wenye ardhi zao hakuna mtu yeyote atakayekuzuia kulima mpaka utakapolipwa fidia,limeni mnapoweza kulima,fanyeni maendeleo yenu pale mnapoweza kufanya muwekezaji atakapokuja sasa tutakuja kwenye hatua ya fidia,lakini tunaogopa kufanya jambo lolote wakati tupo kati kati ya majidiliano,serikali inachukulia hili jambo kwa uzito mkubwa mno"alisema Biteko
Waziri Biteko amesema sababu kubwa ya kuchelewa kuanza kwa mradi wa ligaga na mchuchuma ni pamoja na upitiaji mpya wa mikataba ya miradi baina ya serikali na kampuni ya HOGDA iliyotakiwa kuanza uchimbaji wa madini ya Chuma.
"Baada ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani,serikali iliamua kupitia mikataba mbali mbali na kufanya marekebisho makubwa ya sheria ili kuongeza manufaa kwa watanzania.Mradi huu kama tungeruhusu uende kama ulivyokuwa umepangwa basi watanzania wa Liganga wangebaki maskini mpaka chuma kingeisha lakini Mh.Rais akasema hapana haya madini hayaozi na kama hakuna manufaa ni bora tuchelewe kuchimba kuliko turuhusu wageni waje kubeba rasimali na kuondoka nazo halafu tubaki maskini"alisema Biteko
"Mradi huu una ubia ni ushirika kati ya serikali na wageni,wale wageni wanachukua 80% asilimia 20% ndio ilikuwa inabaki kwenu na katika hilo bado kulikuwa na misamaha mingi ya kodi ambayo nchi isingepata chochote kwa muda mrefu,serikali ikasema hapana lazima tupitie upya mikataba yote,kampuni hii hapa tungeruhusu ichimbe hata ajira zingetoka nje ya nchi na wataalamu wote wasingetoka Ludewa mngekuwa watu wa kushuhudia malori yanakuja hapa na kubeba chuma na kupeleka nje ya nchi,sasa katika utaratibu wa kupitia hii mikataba jambo hili linachukua muda nimesimama hapa kuwaomba kuwa na subira"aliongeza tena Biteko
Vile vile mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka aliendelea kutoa rai kwa wananchi ambao maeneo yao yametambuliwa katika eneo la mradi kuto kukata miti ya asili iliyopo na kupanda mazao ya muda mrefu wakati ukisubiliwa mchakato kukamilika.
Awali wakizungumza na vyombo vya habari wananchi wa kata ya Mundindi,licha ya kuwa na subira wameiomba serikali kuhakikisha wanalipwa fidia zao kwa kuwa maeneo yao mengi yametwaliwa na kusababisha kuto kufanya maendeleo.
"Kwa kweli sisi wananchi tumesimama hatuendi mbele kwasababu ya mradi huu,hatuwezi kufanya kitu chochote katika maeneo haya wengine tangu mwaka 2015 kwa kweli tuomba sana serikali ituaangalie"alisema Gilbeti Mkwawa.
Waziri wa madini Dotto Biteko akizungumza na wananchi wa kata ya
Mundindi waliofika karibu na ofisi za kampuni ya uchimbaji madini ya
HOGDA wilayani Ludewa kusikiliza ujumbe wa waziri juu ya kuendelea kwa
mradi wa Liganga na Mchuchuma.
:Baadhi ya wananchi waliofika katika mradi wa uyeyushaji wa chuma
unaomilikiwa na watafiti wa kuyeyusha chuma na utengenezaji wa zana
mbali mbali za kilimo (Kisangani Black Smith and renawable technology)
wakimsikiliza waziri Biteko kabla ya kuelekea kutazama mradi wa Liganga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...