TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO
VYA HABARI.
KUINGIZA GARI NCHINI
BILA KIBALI.
Jeshi
la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili BAKARI WALII SEMVUA [31] Mfanyabiashara na mkazi wa Mbagala Jijini
Dar -es- Salaam na VICTOR JIMMY BROWN
[25] Dereva/fundi, mkazi wa Tabata Segerea Jijini Dar -es- Salaam kwa tuhuma za
kuingiza Gari nchini bila kibali.
Watuhumiwa
walikamatwa mnamo tarehe 17.03.2020 majira ya saa 19:50 usiku
huko eneo la Mafiati, Kata ya Manga, Tarafa ya Sisimba, Jiji la Mbeya katika
barabara ya Mbeya – Iringa baada ya Jeshi la Polisi kuweka mtego na kufanikiwa
kuwakamata watuhumiwa wakiwa na Gari hilo lenye namba za usajili T.515 DNK aina ya BMW rangi ya
blue na Chassis Namba.WBA 52030CK64536 kutoka nchini Zambia wakiwa
wanaelekea Dar es Salaam.
Baada
ya kuikamata gari na watuhumiwa walifanyiwa mahojiano kwa kuwashirikisha
Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tawi la Mbeya [TRA] upande wa ushuru na forodha na
kubaini kuwa Gari hiyo iliingizwa nchini kama IT na kusafirishwa kupelekwa
Tunduma kwa lengo la kupelekwa nchini Zambia ambapo ilifikishwa mpakani Tunduma
tarehe 07/03/2020 ikiendeshwa na mtuhumiwa BAKARI WALII SEMVUA lakini
ilipofika tarehe 17/03/2020 dereva huyo akiwa na VICTOR JIMMY BROWN
waliamua kuondoka/kuiba Gari hiyo huku wakiwa wameweka “plate” namba T.515
DNK ambayo siyo ya Gari hilo. Upelelezi unaendelea.
KUKAMATWA
KWA WATUHUMIWA WA KUVUNJA GHALA MCHANA NA KUIBA.
Jeshi la Polisi mkoani
Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili [02] FREDY NGODOKI [34]
Afisa Mauzo wa Kampuni ya “Chang Qing” inayojihusisha na utengenezaji,
usambazaji na uuzaji wa Magodoro aina ya Ocean Kiss, Fahari na Okle na THADEI
MATAMBA [30] Mfanyabiashara na Mkazi wa Veta Mbeya kwa tuhuma za kuiba na
kuuza Magodoro 161.
Watuhumiwa walikamatwa
katika msako mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kuanzia tarehe 21.03.2020
na 22.03.2020 katika maeneo ya Jiji la Mbeya, Mbalizi na Itaka Kijiji cha
Ikonya Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa
ambapo FREDY NGODOKI amekiri kuiba magodoro yenye size tofauti 161
yenye thamani ya Tsh. 12, 500, 000/= na kisha kuyauza kwa THADEI
MATAMBA.
Aidha baada ya
mahojiano, mtuhumiwa THADEI MATAMBA amekiri kuuziwa magodoro 143
kwa thamani ya Tsh 10, 000,000/= na kupewa risiti lakini amekiri kuwa
alikuwa bado hajalipa pesa.
Katika msako huo, jumla
ya magodoro 89 yamepatikana nyumbani kwa mtuhumiwa THADEI MATAMBA. Katika
ufuatiliaji mtuhumiwa FREDY NGODOKI amekiri kuuza magodoro mengine 10
huko maeneo ya Uyole. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ULRICH MATEI anatoa wito
kwa wananchi kufuata sheria na taratibu zilizopo ili kujiepusha na
matatizo/usumbufu pindi wanaponunua na kuagiza bidhaa mbalimbali kama vile
magari. Aidha anaendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za
uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na kuchukulia hatua stahiki kwa mujibu
wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...