Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu na wataalam wakiwa wamevalia barakoa (mask) kujilinda na maambukizi ya Kifua Kikuu sugu kabla ya kuelekea kwenye wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ambukizi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu (kushoto) akizungumza na watoto wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu wanaopata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto, Kilimanjaro.
Mkurugenzi,wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi (kushoto) akiwa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya, na Kifua Kikuu wakizungumza na wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi – Kibong’oto.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Dkt. Jasmine Tisekwa (kulia) akizungumza na mtoto Kidawa Baraza mwenye umri wa miaka 10 (kushoto) anayepata matibabu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu Sugu katika Hospitali ya Kibong’oto




Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto Dkt. Riziki Kisongo akisema jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kuu.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi akisema jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu (hawapo kwenye picha) mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Magonjwa Ambukizi (Kibong’oto)
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Mhe. Oscar Mukasa akisema jambo kwa wajumbe wa kamati na wataalam katika kikao mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Magonjwa Ambukizi ya Kibkng’oto. Aliye upande wa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buselu.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Dkt. Mwigulu Nchemba (MB) akichangia hoja katika kikao na wataalam mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi (Kibong’oto) Dkt. Riziki Kisongo akiwaelekeza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu namna ya kuvaa barakoa (mask) kabla ya kuelekea kwenye wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu hospitalini hapo. Aliye upande wa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buselu
……………………………………………………………………………………………………

Na Englibert Kayombo WAMJW – Kilimanjaro.

Tafiti za magonjwa ambuzuki kutoka Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi (Kibong’oto) zimesaidia Shirika la Afya Duniani (W.H.O) kubadilisha miongozo ya kutibu na kugundua vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Riziki Kisongo wakati akiwasilisha taarifa ya Hospitali hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifuaa Kikuu.

Tuna machapisho ya kisayansi 50 ambayo tumeyayachapisha kwenye majarida ya kimataifa, kati ya machapisho hayo; mawili yamechangia kwenye kubadilisha miongozo ya kutibu na kugundua vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu” amesema Dkt. Riziki

“Mwaka 2009 ilikuwa inachukua siku 392 ili mtu kugundulika kuwa ana ugonjwa wa Kifua Kikuu toka aende hospitali’ anasema Dkt. Riziki na kusema kuwa kupitia watafiti waliweza kutengeneza miongozo ambayo ilitoa dira ya kuwa na haja ya kuwa na vipimo vipya ambavyo vingepunguza muda wa kugundua mgonjwa wa Kifua Kikuu.

“Miongozo imesaidia kuja kwa vipimo vya kisasa vya ugonjwa wa Kifua Kikuu “GeneXpert Mashines” ambazo zinachukua masaa mawili na nusu kepee kufanya vipimo vya ugonjwa wa Kifua Kikuu” Amesema Dkt. Riziki.

Andiko lingine lililobadili tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu amesema kuwa kupitia machapisho hayo, tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu imebadilika na sasa wagonjwa wanatibiwa kupitia dawa na sii sindano kama ilivyokuwa awali.

“Tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu ilikuwa ni kwa njia ya sindano kwa muda wa miezi nane, utafiti ulivyofanyika hapa ilionekana asilimia 47 ya wagonjwa walikuwa wanapata matatizo ya usikivu” anasema Dkt. Riziki na kuendelea kusema kuwa kwa kuchapisha maandiko hayo yalisaidia kubadili tiba ya ugonjwa huo ambapo hadi hivi sasa tiba inatolewa kwa vidonge.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi inayofanya vizuri kwenye matibabu ya TB ambapo hadi hivi sasa ina vituo 145 vya matibabu ya Kifua Kikuu sugu nchi nzima, tofauti na awali ambapo ilikuwa na Hospitali ya Kibong’oto pekee.

“Lengo la kuwa na Hospitali ya Kibong’oto sio kwa ajili ya kutoa tiba pekee bali wanatakiwa kubobea kwenye tafiti, tiba na matokeo chanya kwa Taifa na Dunia kwa ujumla” amesema Dkt. Subi na kuendelea kusema kuwa Wizara ya Afya imeongezewa uwezo Hospitali hiyo wa kushughulikia magonjwa yote ambukizi, tafiti na ufuatiliaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Mhe. Oscar Mukasa amefurahi kusikia Hospitali hiyo inatoa mchango wa mabadiliko ya sera za matibabu ya magonjwa kutokea Tanzania na kuwasihi waongeze juhudi zaidi na kuja na tafiti nyingi zaidi zitakazo saidia katika kupata tiba ya ugonjwa huo ambao bado ni tatizo kubwa kwa Watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...