MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO), Dkt. Alexander Kyaruzi amesema ndani ya kipindi kifupi kijacho cha kuanzia sasa mpaka Desemba 2020 mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma itakuwa na imeme wa kutosha.
Hiyo ni baada ya kukamilika kwa Ujenzi wa Miradi mikubwa ya kusafirisha umeme wa gridi ya Taifa kuanzia Bulyanhulu mpaka Geita, Geita mpaka Nyakanazi na ule wa Nyakanazi mpaka Rusumo ikitekelezwa sambamba na miradi ya kufua umeme wa maji ya Rusumo na Malagarasi na hivyo kuwataka Wananchi na Wawekezaji kwa ujumla kujipanga kuwekeza na kuchangamkia fursa zinazopatikana maeneo ya Mikoa hiyo kwa wingi bila kusita kutokana na fursa ya upatikanaji wa umeme mwingi na wauhakika.
Dkt. Kyaruzi aliyasema hayo wakati wa ziara ya bodi ya wakurugenzi TANESCO ilipotembelea na kukagua maendeleo ya miradi hiyo.
“Muwekezaji yeyote yule asiwe na wasiwasi sasa Tunajenga laini za kusafirisha umeme mkubwa wa msongo wa kilovilti 220 kutoka Bulyanhulu mpaka Geita, Tukitoka Geita tunakwenda Nyakanazi na kutoka Nyakanazi tutakwenda Rusumo ambapo tutapata umeme wa megawati 27 pia tutajenga laini nyingine kwenda kigoma ambapo tutapata umeme wa megawati 45 kutoka kwenye mradi wa bwawa la Malagarasi,” amesema Dkt. Kyaruzi
Aidha Bodi hiyo ya Wakurugenzi ya TANESCO ikikagua miradi hiyo, ilishauri na kuagiza utekelezaji wa mambo mbalimbali ambayo yataongeza ufanisi na kasi ya utekelezaji miradi hiyo kwa ubora uliokusudiwa Ikiwemo, umakini katika ukaguzi na uthibitishaji wa ubora wa vifaa kulingana na mkataba, Kuzingatia muda wa ukanilishaji mradi bila kuchelewa, kuzingatia uzito wa vifaa vya mradi vinavyosafirishwa toka bandarini kuja eneo la mradi kuepuka madeni ya faini zitokanazo na kuzidisha uzito barabarani.
Wakati huo huo, naye msimamizi wa Miradi Toka TANESCO, Mhandisi Florence Gwang’ombe alielezea shauku kubwa ya TANESCO kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo yote kwa wakati na kwa viwango na ubora uliokusudiwa ili kufanikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika utakaochochea maendeleo na uwekezaji katika Mikoa ya kanda ya Ziwa na ile ya Kaskazini Magharibi mwa Nchi.

Wajumbe bodi ya Wakurugenzi katika Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) wakiwa katika ziara ya kukagua mradi wa umeme
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...