Wana CAMA ni mtandao wa wasichana
waliofadhiliwa na shirika la CAMFED kupata elimu. Katika kudhimisha siku ya
Wanawake Duniani wana CAMA walijumuika na wanawake wengine katika wilaya za
Kilosa, Gairo, Morogoro, Ifakara,
Kilombero, Kibaha, Chalinze, Rufiji, Kibiti, Kilolo, Handeni DC, Handeni TC, Iringa
na Pangani, kuadhimisha siku hiyo kwa
kishindo.
Baadhi ya mabinti waliofadhiliwa na CAMFED (wana
CAMA) kusoma ufundi wa magari katika
chuo cha wananchi Handeni (Folk Development Collage) wakionyesha uwezo wao
katika madhimisho ya siku ya wanawake wilayani Handeni.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro mjini Bi. Regina
Chonjo akipokea msaada wa mabox ya taulo za kike uliotolewa na wafadhiliwa wa
CAMFED (wana CAMA) wa wilaya ya Morogoro kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake
wilayani Morogoro. Huu ni utaratibu waliojiwekea wana CAMA hawa kuhakikisha
wanarudisha mafanikio yao kwenye jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Bi. Asiah Abdallah
aliyekua mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wilayani kilolo
akitazama bidhaa za mafuta ya kupikia zinazozaliswa na wana CAMA wa wilaya ya
kilolo.
Baadhi ya wana CAMA kutoka wilaya
mbalimbali hawakubaki nyuma katika kuonyesha umahili wakutengeneza bidhaa
mbalimbali zikiwemo asali, unga wa ugali, na utengenezaji wa chaki.
Wana CAMA walikua pia na ujumbe wakumlinda
mtoto wa kike kuhakikisha anafikia ndoto zake.
Baadhi ya wasichana waliofadhiliwa na
CAMFED (wana CAMA) kusoma ufundi wa umeme katika chuo cha
wananchi Handeni (Folk Development Collage) wakionyesha uwezo wao katika
madhimisho ya siku ya wanawake wilayani Handeni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...