Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amesema mkoa huo utaanza rasmi kesho zoezi la kupuliza dawa ya kuua vijidudu na kudhibiti kuenea kwa Virusi vya Corona katika maeneo mbalimbali ya Jiji hilo ambapo amewataka wananchi wasiwe na hofu pindi wanapoona magari yanapita mitaani kupuliza dawa.

RC Makonda amesema kwa kufanya hivyo  itasaidia pia kuua Vimelea na Wadudu kama Mbu wanaoenzeza ugonjwa wa Malaria, homa ya dengu na magonjwa mengineyo na kufanya jiji hilo kuwa katika hali nzuri ya kuwakinga wananchi wake.

Mhe. Makonda amesema hayo wakati alipofanya Ziara kwenye Maeneo yanayopokea Wasafiri kutoka nje ya Nchi ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo na Bandarini kwa lengo la kukagua namna walivyojipanga kudhibiti kuenea kwa Virusi Vya Corona ikiwemo namna ya wanavyowahudumia Wasafiri kuanzia Vipimo.

Aidha RC Makonda ameonyesha kuridhishwa na namna taasisi hizo zimejidhatiti kuwahudumia Wasafiri kutoka Ndani na Nje ya Nchi kuanzia unawaji wa mikono na kuchukuliwa vipimo vya joto ambapo amewahimiza kuhakikisha kila mgeni anaeingia Nchini anachukuliwa na kuwekwa kwenye uangalizi kwa siku 14.

Pamoja na hayo RC Makonda amewaelekeza wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi kuhakikisha wanaweka Vyombo vya kunawa mikono mwanzo wa safari na mwisho wa safari ikiwa ni pamoja na kufanya usafi wa gari kila Mara.

Hata hivyo RC Makonda amewataka Wananchi kuendelea kujikinga na Virusi vya Corona kwa kunawa nikono na maji yenye Dawa, kuepuka kujazana kwenye vyombo vyaVvu usafiri, kuepuka safari zisizo na ulazima pamoja na kuepuka Mikusanyiko.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kulia) akizungumza na waandishi wahabari leo March 24, 2020 kuhusu zoezi la kupuliza dawa ya kuua vijidudu na kudhibiti kuenea kwa Virusi vya Corona katika maeneo mbalimbali ya jiji la  Dar es Salaam,ambapo amewataka wananchi wasiwe na hofu pindi wanapoona magari yanapita mitaani kupuliza dawa.(Picha  zote na Emmanule Massaka wa Michuzi Tv)

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na abilia (hawaapo pichani) katika Uwanja wa Ndege wa  Kimatafa wa Mwalimu Julius Nyerere.


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (katika) akiendelea na ziara katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  katika ziara ya  kukagua kwenye Maeneo yanayopokea wasafiri kutoka nje ya  Nchi ikiwemo Uwanja wa Ndege wa  Kimatafa wa Mwalimu Julius Nyerere, Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo na Bandarini kwa lengo  kuona namna walivyojipanga kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (katikati) akizungumza na abilia ndani ya Mabasi  kaitika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo na kuona namna walivyojipanga kudhibiti kuenea kwa Virusi vya Corona, leo March 24, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kushoto) akiendelea na ziara  kaitika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo na kuona namna walivyojipanga kudhibiti kuenea kwa Virusi vya Corona, leo March 24, 2020.
Mabasi yakiwa kaitika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo.(Pichz zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...