Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi (MB) wa Mkuranga,Abdallah  Ulega amefanya ziara kukagua miundombini mbalimbali katika kijiji cha Msonga kata ya Msonga Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ili kujionea changamoto iliopo wilayani hapo ya barabara kutokana na mvua zilizonyesha maeneo mbalimbali nchini.

Ulega amesema Mkuranga kuna changamoto ya mvua zilizoungana toka tarehe 5 mwezi wa 10 mwaka jana (2019) mpaka sasa mvua bdo zinaendelea kunyesha na kupelekea hali ya miundo mbinu kuwa ngumu.

"Upande wa kata ya Msonga mawasiliano ya kata kwenda wilayani yamekuwa magumu na imenilazimu kama mbunge kuja kuona hali halisi" Ulega.

Aidha Ulega ametoa maelekezo kwa Meneja wa TARURA wa Wilaya kuhakikisha inapatikana suluhu ya dharura juu ya jambo hilo, utaratibu wa kuandika maandiko ya kwenda ngazi za Taifa kuona ni kwa namna gani uwezekano wa msaada wa kutatua tatizo hilo umeshafanyika.

Ulega alimaliza  kwa kusema " vilevile nimekagua shughuli za kimaendeleo za kata hii ya Msonga, ujenzi wa ofisi ya mtendaji wa kata ya Msonga kijiji cha Msonga jengo la Chama Cha Mapinduzi ya kata ya Msoga na zahanati ya kijiji cha Msonga ambayo tumeianzisha wenyewe.
Ni matumaini yetu kuwa kazi hii ya kuchimba msingi itaungwa mkono na hatimaye kumaliza ujenzi kwa haraka.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi( Mb) wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akikagua  daraja kijiji cha Msonga  kata ya Msonga wilaya ya  Mkuranga mkoa wa Pwani limesombwa na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano katika ziara kukagua miundombini mbalimbali.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)


Muonekano wa Daraja la kijiji cha Msonga  kata ya Msonga wilaya ya  Mkuranga mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi( Mb) wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega (kushoto)akizungumza na waananchi wa kijiji cha Msonga kata ya Msonga wialya ya Mkuranga mkoa wa Pwani katika ziara kukagua miundombini mbalimbali.




Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi( Mb) wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akiwasikilza kwa makini wazee wa kijij cha Msonga kata ya Msonga wila ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Msonga  ukiendela 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...