Na Kijakazi Abdalla
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema itaanza mpango wa kuzitoza
kodi baadhi ya makampuni ambazo hazilipi kodi kwa kisingizio cha
kupata hasara katika biashara zao.
Hayo ameyasema Afisa Mwandamizi wa Huduma na Elimu kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) kwa upande wa Zanzibar Shuweikha Salum Khalfani
huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo wakati akiwasilisha mada ya taarifa za
Mapato ambayo imewashirkisha watembezaji watalii.
Amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya ulipaji kodi kwa baadhi ya
makampuni kutolipa kodi kwa kisingizio cha kupata hasara kwa biashara
zao.
Aidha amesema kuwa ulipaji wa kodi hiyo utakuwa ni asilimia 0.5 ya
mauzo ya mwaka kwa makampuni ambayo yamepata hasara kwa miaka mitatu
mfululizo.
Pia amesema sheria ya mapato ya 2004 imeeleza kuwa kodi ya mapato ya
biashara au uwekezaji itatathiminiwa na inapaswa kulipwa kila mwaka wa
mapato kwa mtu binafsi au kampuni.
“ sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015 imemtaka mtu yoyote
anayefanya uwekezaji au biashara ajisajili TRA na kupatiwa utambulisho
wa mlipa kodi ndani ya siku 15 baada ya kuanza biashara au
uwekezaji”amesema afisa muandamizi huduma na elimu.
Vilevile Afisa huyo ameelezea kuwa tafiti nyingi duniani zinaonesha
kuwa Serikali mapato yake yanatokana na ulipaji kodi na sio wahisani
wala mikopo.
Amesema kuwa Serikali hutumia kodi kwa kugharamia huduma mbalimbali
zinazotolewa kwa jamii kama vile ulinzi,elimu,afya na miundo mbinu.
Nao washiriki wa semina hiyo wameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kuunda sherian itayowabana wale
ambao wanatembeza watalii bila ya kulipa kodi .
Aidha wamesema Serikali inategemea zaidi mapato kutoka sekta ya utalii
lakini kumekuwepo na baadhi ya watembezaji watalii hawalipii kodi.
Afisa Mwandamizi wa Huduma na Elimu TRA Shueikha Salum Khalfan akitoa mada kuhusiana na Taarifa za Mapato kwa watembezaji Watalii katika hafla ya Uwasilishaji Taarifa za Mapato iliofanyioka katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Baadhi ya Wageni Waalikwa waliohudhuria katika hafla ya Uwasilishaji Taarifa za Mapato iliofanyioka katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Katibu ZATO Omar Makame Kali akitoa ushauri kwa maafisa
mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya Uwasilishaji Taarifa za
Mapato iliofanyioka katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA/MAELEZO ZANZIBAR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...