Charles James, Michuzi TV
KATIKA kusherehekea siku ya wanawake duniani, Wafanyakazi Wala ya kazi wanawake wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wametembelea kituo cha watoto yatima cha Rahman kilichopo jijini Dodoma na kuwapa misaada mbalimbali.

Wafanyakazi hao kwa umoja wao wamepeleka Mabati, Mbao, Mifuko ya Saruji, Misumari na Milango kwa ajili ya kumalizia baadhi ya mabweni lakini pia walibeba vyakula kama Mchele, Mafuta ya kupikia, Maji na Juisi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa kituo hicho, Mgeni rasmi kutoka Tanesco Makao Makuu, Injia Sophia Mgonja amesema wao kama akina mama wameona ni vema kusherehekea sikukuu ya wanawake kwa kuungana na Watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Amesema wanaamini vifaa hivyo vitasaidia katika hatua ya ujenzi iliyobaki ili kituo hiko kiweze kupata majengo mengi yatakayoweza kubeba watoto wengi zaidi kulinganisha na sasa.

" Niupongeze uongozi wa kituo hiki kwani kazi hii mnayofanya ni ya wito na ni Mungu pekee ambaye anaweza kuwalipa. Sisi tuwatie moyo na tunaahidi kwamba hatutoishia leo tutakuja kadri tutakavyojaliwa," Amesema Mgonja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyakazi hao, Renilda Kageuke amesema waliguswa kuchangia ujenzi wa jengo hilo baada ya kuliona na kumuahidi Mkuu wa kituo hiko kwamba wataendelea kushirikiana nao kila mara.

" Sisi wanawake wafanyakazi wa Tanesco tumeona ni vema tuje kula na kusherehekea na Watoto wetu hapa, lakini tukaona ni vema tuje na vitu ambavyo vitakua na faida kwenye kituo hiki kwa miaka mingi ijayo.


Hivyo tumebeba mabati 100, mifuko 60 ya safuji, mbao 160, Milango sita, mbao za kupaua, misumari pamoja na vyakula, huu siyo mwisho tutaendelea kushirikiana nanyi kadri tutakavyojaliwa," Amesema Renilda.

Nae Mkuu na Mwanzilishi wa kituo hiko, Bi Rukia Hamis amewashukuru akina mama hao kwa moyo wao wa kusaidia huku akisema vifaa hivyo vya ujezi vitakua msaada mkubwa katika kumalizia mabweni yao.

Akisoma historia ya kituo hiko amesema kilianzishwa mwaka 2006 likiwa na watoto 12 lakini leo hii wameongezeka hadi watoto 40 ambao wanalala hapo hapo na 15 wengine wakiwa wanatokea kwa walezi wao.

" Hakika mmetushika mkono tunaomba na wadau wengine waje kutusaidia pale watakapoguswa. Hicho ni kituo ambacho kimekua msaada kwa watoto wengi na ili tuendelee tunahitaji kushikwa mkono.

Tumepata mafanikio makubwa hapa wapo watoto waliomaliza shule wakiwa hapa, wengine wamepata kazi lakini zaidi tunae mwanafunzi mmoja anaitwa Yusuf anasoma Chuo Kikuu cha Sudan akiwa mwaka wa pili," Amesema Bi Rukia.

Mmoja  wa watoto wanaoishi kwenye kituo hiko amewashukuru wafanyakazi hao na kuwataka kuendelea kusaidia watoto na watu wengine wenye mazingira magumu bila kuchoka.
 Viongozi wa Umoja wa Wafanyakazi Wanawake wa Shirika la Umeme nchini Tanesco wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima cha Rahman pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa kituoni hapo ambao wafanyakazi hao wa Tanesco wametembelea kituo hiko na kutoa misaada mbalimbali.

Mwakilishi wa Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco Makao Makuu akizungumza na Watoto na walezi wa kituo cha watoto yatima cha Rahman kilichopo eneo la Chang'ombe jijini Dodoma.
 Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hiko cha Rahman akitoa shukrani zake kwa wafanyakazi wanawake wa Tanesco waliofika kituoni kwao kuwapatia misaada.
 Muonekano wa jengo la bweni la kituo cha kulelea watoto yatima cha Rahman ambacho wafanyakazi wanawake wa Tanesco wamekitembelea na kuwapatia msaada wa vifaa vya ujenzi.
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco kushoto wakiwa na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Rahman walipofika kukitembelea na kuwapatia msaada mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...