WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka wananchi washirikiane na Serikali katika kuwafichua wafanyabiashara wa magendo wanaoingiza bidhaa kwa kupitia bandari bubu.
Pia ameiagiza Idara ya Uvuvi wilaya ya Pangani ihakikishe inadhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu na nyavu zisizo stahili kwa kuwa unahatarisha mazalia ya samaki.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 6, 2020) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Bomani, wilayani Pangani.
Amesema uwepo wa bandari bubu katika wilaya hiyo unasababisha kuingizwa kwa bidhaa ambazo viwango vyake havijathibitishwa na mamlaka husika hivyo kuhatarisha afya za watumiaji.
“Wananchi shirikianeni na Serikali katika kuwataja wanaoingiza bidhaa kupitia bandari bubu kwani licha ya bidhaa hizo kutokuwa na uhakika wa ubora, pia hata wakwepakodi nao wanapitia huko.”
Kadhalika, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu malalamiko ya wafanyakazi wa mkonge ambapo amesema atamuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama aende kushughulikia suala hilo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameishukuru Serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, maji na umeme kwani kati ya vijiji 33 vya jimbo hilo vitatu tu ndio havina umeme.
Pia mbunge huyo ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali iharakishe utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani yenye urefu wa kilometa 50 pamoja na ulipaji fidia kwa wananchi wanaotakiwa kupisha mradi huo.
Awali, Waziri Mkuu alizindua mradi wa ujenzi wa ujenzi wa ukuta wa mto Pangani kwa upande wa kaskazini wenye urefu wa mita 950 uliogharimu sh. Bilioni 2.9. Pia alizindua kituo cha polisi cha wilaya ya Pangani pamoja.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua mradi wa ujenzi wa ukuta wa mto
Pangani akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga Machi 6, 2020. Kulia ni
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, wa pili kulia ni Naibu Waziri, Ofisi
ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira, Mussa Sima na kushoto ni Mkuu
wa wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa ujenzi wa ukuta wa mto
Pangani kabla ya kuuzindua ukuta huo, Machi 6, 2020. Kushoto ni Naibu
Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Sima na
kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zaibab Abdallah Issa.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitia saini kitabu cha wageni akiwa kwenye
Ofisi ya Mkuu wa polisi wa wilaya ya Pangani, Georgina Matagi (kulia)
wakati alipozindua kituo kipya cha Polisi cha wilaya ya Pangani, Machi
6, 2020. Kituo hicho kimejengwa uhamasishaji uliofanywa na Mkuu wa
Polisi wa wilaya hiyo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye
uwanja wa Bomani Pangani akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga, Machi 6,
2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi
wa Pangani wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Bomani Pangani akiwa
katika ziara ya mkoa wa Tanga Machi 6, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...