Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza na wakimbizi wa Burundi waliohifadhiwa katika Kambi ya
Nduta iliyoko wilayani Kibondo, mkoani Kigoma na kuwataka kujiepusha na
uhalifu pamoja na kuwaficha wahalifu ndani ya kambi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea salama ya heshima baada ya
kuwasili wilayani Kibondo kutembelea Kambi ya Nduta iliyoko mkoani
Kigoma na kuwataka wakimbizi katika kambi hiyo kujiepusha na uhalifu
pamoja na kuwaficha wahalifu ndani ya kambi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiongozana na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya
Kibondo, Kanali Hosea Ndagala (kulia) baada ya kuwasili wilayani
Kibondo kutembelea Kambi ya Nduta, mkoani Kigoma na
kuwataka wakimbizi katika kambi hiyo kujiepusha na uhalifu pamoja na
kuwaficha wahalifu ndani ya kambi.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibondo,
Kanali Hosea Ndagala akitoa taarifa ya hali ya Ulinzi na Usalama ya
wilaya yake wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (aliyekaa kiti cha mbele), kutembelea Kambi ya
Nduta, mkoani Kigoma na kuwataka wakimbizi katika kambi hiyo kujiepusha
na uhalifu pamoja na kuwaficha wahalifu ndani ya kambi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
…………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu,Kibondo
Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameviagiza Vyombo vya
Ulinzi na Usalama mkoani Kigoma kuwaondosha na kuwafungulia mashtaka
wakimbizi zaidi ya Elfu Moja waliotoroka kutoka katika Kambi mbalimbali
za wakimbizi na kwenda kufanya uhalifu nje ya makambi.
Naibu Waziri
Masauni ameyasema hayo leo wakati akiongea na wakimbizi kutoka nchini
Burundi waliohifadhiwa katika Kambi ya Nduta iliyoko wilayani Kibondo,
mkoani Kigoma huku ikihifadhi jumla ya wakimbizi na waomba hifadhi
75,055.
“Tanzania na
Burundi zimekua zikishirikiana kwa muda mrefu,Tanzania si nchi ya
kubembeleza watu waovu na haijawahi kufuga wahalifu , kuna watu zaidi ya
Elfu Moja wamevunja sheria za ukimbizi kwa kutoroka kwenye makambi na
kwenda kufanya uhalifu huko nje, sasa naviagiza vyombo vya usalama
kuhakikisha wanawaondosha hao watu kwa mujibu wa sheria na itakua
fundisho kwa watu wote wenye tabia ya kutoroka makambini na kwenda
nje kufanya uhalifu, ” alisema Masauni
Masauni pia
aliwataka wakimbizi hao kuendelea kujiandikisha kwa hiari ili waweze
kurudi nchini kwao Burundi ambako hali ya amani sasa imerejea na tayari
pande tatu ikiwemo Serikali ya Tanzania, Serikali ya Burundi na Shirika
la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) washatiliana saini mkataba
utakaofanikisha zoezi hilo kwa wanaotaka kurejea Burundi
“Serikali ya
Burundi imetuthibitishia kurejea kwa amani katika nchi yenu, nendeni
mkaijenge na kuitumikia nchi yenu, nchi yoyote ili iweze
kuendelea inahitaji watu na hapa naona kuna vijana wengi tu ambao ndio
msingi wa maendeleo wa nchi yoyote ile duniani”aliongeza Masauni
Akizungumza
katika Mkutano huo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Kanali Hosea
Ndagala aliwataka wakimbizi hao kufuata sheria za nchi na wao kama
Kamati ya Ulinzi na Usalama watahakikisha kila atakaethibitika kufanya
uhalifu sheria itachukua mkondo wake ikiwemo kufutiwa ukimbizi na
kufunguliwa mashtaka.
“Hatutoruhusu mtu
yoyote kuingiza vitu visivyoruhusiwa katika makambi ambavyo vinaweza
kuhatarisha usalama katika makambi yenu na tunaomba mkiona kitu chochote
kisicho cha kawaida mtoe taarifa kwa viongozi ili mbakie katika
mazingira salama” alisema Kanali Ndagala
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti katika mkutano huo wakimbizi hao waliishukuru Serikali
ya Tanzania kwa kuwahifadhi na kuwapa huduma ya ulinzi huku wakiomba
kuwahishiwa huduma mbalimbali ikiwemo nguo,chakula na huduma za afya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...