Na Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Wiki ya msaada wa Sheria imezinduliwa Mkoani Kagera Wilayani Karagwe na Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti katika Viwanja vya Changarawe Wilayani humo, lengo likiwa ni kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi hususani makundi maalumu.

Uwepo wa huduma hii itakayotolewa katika Wilaya za Karagwe, Ngara na Biharamlo Mkoani Kagera inafanyika wakati ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imekuwa ikipokea kwa wingi malalamiko ya Wananchi wanaohitaji msaada wa Kisheria ambapo wahanga wa sheria wamekuwa wakitokea maeneo mbalimbali Mkoani humor, kutaka msaada katika nyanja za Kijamii, kisiasa na hata kiuchumi Hivyo kufuatia kusogezwa kwa huduma hiyo kutasaidia kutanzua changamoto zinazokabili mamia ya wananchi hao.

"Pale kwangu ofisini nimekuwa nikipokea kwa wingi watu wengi wa aina mbalimbali, wengi wao ni wale ambao wamekuwa wakihitaji msaada wa kisheria katika masuala mbalimbali, na wengine imefikia hatua wanakuwa hawana hata nauli ya kurudi makwao hivyo Ofisi inalazimika kuwatafutia nauli, hii ni jinsi gani msaada wa kisheria unahitajika sana.." Amenukuliwa Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati wa uzinduzi huo.

Kwa upande wao waandaaji wa Wiki hiyo TANLAP chini ya ufadhili wa UNWOMEN, Afisa mradi Ndg. Mchereli Machumbana ameitaja wiki msaada wa kisheria kuwa na nia ya usawa wa huduma ya kisheria na usawa wa kijinsia unafikiwa kupitia Sera mikakati pamoja na bajeti inayopangwa na Serikali, Akiongoza kuwa Mwaka 2018 TANLAP walipata mradi wa kupinga Ukatili wa Kijinsia kupitia msaada wa kisheria ambao umetekelezwa vyema katika Mkoa wa Kagera na kuomba ushirikiano pindi Mradi huo ukianza kutekelezwa kwa awamu ya pili.
 Wananchi Wilayani Karagwe wakionekana katika mistari wakisubiri huduma ya kusikilizwa masuala yahusuyo sheria, katika uzinduzi wa Wiki ya Msaada wa Sheria Wilayani Karagwe.
 Pichani ni Ndg. Mchereli Machumbana, Afisa mradi - TANLAP, ambao ndio waandaaji wa Wiki ya Huduma ya Msaada wa Kisheria, chini ya Ufadhili wa UNWOMEN akitoa salaamu zake wakati wa uzinduzi wa Wiki ya huduma ya Msaada wa Sheria.
 Pichani mwenyekiti wa Akina mama Wajane Bi Grace Mahumbuka (Mama Meneja) akitoa ushauri wake wa namna ya usaidizi wa masuala mbalimbali yanayolikabili kundi kubwa la akina mama hao wajane.
 Pichani ni Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco  E. Gaguti akitoa mwongozo na ufafanuzi juu ya uwepo wa Wiki ya msaada wa Sheria lengo likiwa ni kupata majibu ya changamoto za kisheria
 Pichani ni Mkuu wa Wilaya Karagwe Godfrey Mheluka akimtembeza Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jen. Marco Gaguti katika magazebo ya wadau wa sheria, na hapo ni katika gazebo LA WOMEDA
 Pichani ni Ndg. Mchereli Machumbana, Afisa mradi - TANLAP, ambao ndio waandaaji wa Wiki ya Huduma ya Msaada wa Kisheria, chini ya Ufadhili wa UNWOMEN akitoa salaamu zake wakati wa uzinduzi wa Wiki ya huduma ya Msaada wa Sheria.
 Pichani ni maafisa wa TAKUKURU wakiendelea kutoa Elimu na ufafanuzi kuhusu masuala ya Rushwa kwa Mwananchi aliyefika hapo kutaka kufahamu masuala ya kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...