Na
Amiri kilagalila,Njombe
Wakati
baadhi ya wanawake wakiungana mkoani Njombe kuadhimisha siku ya wanawake
duniani inayotarajiwa kufikia kilele chake hapo machi 8 mwaka huu,wananchi
wametakiwa kuacha tabia ya kukataa kujitokeza kutoa ushahidi mahakamani ili
kukamilisha upelelezi utakaosaidia kupunguza msongamano wa mahabusu na wafungwa
gerezani.
Kwa
niaba ya mkuu wa wilaya ya Njombe katibu tawala wilaya bwana Emmanuel George
baada ya kufika katika gereza la wilaya ya Njombe (Mpechi) na kukabidhi baadhi
ya msaada wa vitu muhimu kama mafuta huku akiongozana na wanawake wanaoendelea
kufanya shughuli mbalimbali kuelekea siku ya wanawake duniani amesema kuwapo
kwa msongamano mkubwa wa mahabusu na wafungwa unasababishwa na jamii kuto
jitokeza kutoa ushahidi wakati wa kesi mahakamani.
“Njombe
watu hawatoi ushirikiano ili kesi ziishe haraka lakini ni rai yangu kutoa
ushahidi wa haraka ili kupunguza idadi ya mahabusu kwenye magereza yetu lakini
niwapongeze uongozi wa gereza kwa kuwatengeneza hawa watu kisaikolojia”alisema
Emmanuel George
Lilian
Nyemele ni katibu tarafa wa Njombe mjini aliyeongozana na wanawake wenzake
kutoa misaada mbalimbali huku akisema kupitia muendelezo wa kuelekea kilele cha
siku ya wanawake duniani anasema wameguswa na kundi la mahabusu wanawake na
kuona umuhimu wa kwenda kuwashika mkono.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa gereza la wanawake Njombe askari Theresia Kiswaga anasema
kitendo kilichofanyika na wanawake hao kinafaa kuigwa katika jamii kwani vitu
walivyowapa mahabusu na wafungwa vitawasaidia sana kuwapunguzia ukali wa maisha
ndani ya gereza hilo.
“Lakini
pia tunaendelea kutoa wito kuendelea kututembelea sio tu kusubiri
sherehe,tunaomba hata siku ya jumamosi au jumapili kuja kuwaona hawa ndugu zetu
na hata siku za sikuku za kitaifa,vifaa vilivyotolewa vitakuwa na msaada kwetu
kwa mfano maziwa kwa ajili ya watoto hapa sisi hatuna mifugo lakini mmetuletea
maziwa tunashukuru”alisema Thelesia Kiswaga
Kwa
upande wake mkuu wa gereza la wilaya ya Njombe SSP Charles Mhinga amekiri kuwa misaada hiyo ni upendo
tosha uliopo baina ya wanawake na ndugu zao waliopo katika mazingira magumu ya
gerezani.
“Nimefarijika
sana kwa misaada hii ambayo akina mama kwa umoja wao wamekuja kuwasilisha kwa
wamama wenzao ambao wapo katika mazingira haya,uhitaji upo lakini sisi
tunashukuru kwa hili”alisema Cherls Mhina
Miongoni
mwa misaada iliyotolewa na akina mama mkoani katika gereza hilo ni pamoja na
Sabuni,taulo za kike,ndala ,mafuta na hata mavazi mabali mbali
bado
shughuli mbalimbali zinaendelea kufanyika na wanawake hao ikiwemo kufanya
maonesho ya bidhaa katika viwanja vya turbo mjini Njombe huku wito ukitolewa
kwa jamii kujitokeza kuwaunga mkono wanawake katika nyanja mbalimbali.
Baadhi ya viongozi na wanawake wakisalimiana baada ya kufika gereza la
mpechi kwa ajili ya kutoa misaada
Akina mama na viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa
Magereza mara baada ya kuwatembelea mahabusu na wafungwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...