NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo
cha Sharom kilichopo kata ya Msangani Wilayani Kibaha Mkoani Pwani
wamemuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwasaidia kwa hali na mali
kuwasaidia kuwatatulia changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo
ukosefu wa mahitaji ya chakulai,nguo, huduma za matibabu pamoja na
ujenzi wa jengo la nyumba kwa ajili ya kuweza kuishi.
Baadhi ya watoto hao akiwemo Sara Yendemba Dickson Michael na
wakizungumza wakati wa halfa ya kupokea msaada wa mahitaji mbali mbali
ikiwemo chakula kutoka kwa kikundi cha Pwani Generation mwanamke
sahihi walisema kwamba baada ya kuondokewa na wazazi wao wamekuwa
wanaishi katika mazingira magumu na wakati mwingine walikuwa
wanakwenda kutafuta chakula majalalani hivyo wanahitaji msaada wa hali
na mali kutoka serikalini na wadau wengine wa maendeleo ili waweze
kujikimu kimasiha kama watoto wengine.
“Tunashukuru sana kwa msaada wa vyakula mbali mbali ambavyo tumepatiwa
na uongozi wa wanawake wa Pwani Generation kwani utaweza kutusaidia
kwani sisi hapa ni watoto yatima na wengine tunaishi katika mazingira
magumu, lakini kitu kikutu bado tunamuomba Rais wetu aweze kutusaidia
zaidi ujenzi wa nyumba ya kulala kwani idadi yetu ni kubwa kuliko
vitanda vilivyopo”walisema watoto hao kwa masikitiko makubwa.
Pia waliongeza kwamba kabla ya kufikishwa katika kituo hicho walikuwa
wanaishi mitaani kwa shida kubwa sana kutokana na kukabiliwa na
changamoto mbali mbali ya kukosa mavazi, chakula sambamba na mambo
mengine muhimu lakini kutokana na kituo hicho angalau wameweza
kupatiwa hata fursa ya kwenda shule ya ajili ya kupata elimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation mwanamke
sahihi Betty Msimbe amesema kwamba wameamua kutoa msaada huo wa
mchele, mafuta, unga, sukari, pamoja na maharage katika kituo hicho
kutokana na kubaini kuwepo kwa changamoto nyingi ambazo zinawakabili
watoto hao ambao wanahitaji kusaidiwa mahitaji mbali mbali ili weze
kujikimu kimaisha.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba katika kikundi chao wamekuwa na
utaratibu wa mara kwa mara kwenda kutoa misaada katika vituo mbali
mbali vya kulelea watoto yatima na wale wanaosihi katika mazingira
magumu vilivyopo katika Mkoa wa Pwani lengo ni kuwapatia mahitaji
muhimu ambayo wanastahili pamoja kwenda kuwafariji.
“Sisi kama Pwani Generation mwanamke sahihi tumeweza kubaini kuwa
kituo hiki cha Sharom ambacho kipo katika Wilaya ya Kibaha bado
kinakabiliwa na changamoto mbali mbali na ndio maana tukaamua
kujikusanya fedha na kuamua kununua mahitaji mbali mbali ambayo
wanastahili kupatiwa watoto hao kwani kutoa ni moyo na wala sio
utajiri hivyo ni moja ya kuunga mkoni juhudi za serikali katika
kuwasaidia watoto,”alisema Msimbe.
Naye mlezi wa Kituo hicho Lilian Mbise ambaye pia na yeye ni yatima
amesema kwamba kituo hicho ambacho kilianzshiwa tangu mnamo mwaka 2016
kina watoto wapatao 18 ambao wanaishi katika nyumba ya kupanga hivyo
kunahitajika msaada zaidi kutoka serikalini kwa lengo la kuweza
kuzitatua changamoto hizo zinazowakabili kwani mahitaji yao ni mengi.
Kikundi hicho cha Pwani Generation mwanamke sahihi kilitoa msaada wa
vitu mbali mbali mbali ikiwemo unga wa sembe, sukari, mafuta ya kula,
mchele,maji pamoja na mahitaji mengine ya msingi kwa ajili ya watoto
yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Sharoom
ambapo vimegharimua kiasi cha zaidi ya shilingi milioni moja.
Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi wa kushoto akimkabidhi msaada wa vyakula mbali mbali Lilian Mbise ambaye ni Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu cha Sharom kilichopo katika eneo la Kwa mathiasi kata ya Msangani Wilayabi Kibaha,katika halfa iliyofanyika katika kituo hicho.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mlezi wa kituo cha Sharom cha kulelea watoto yatima na wale wanaosihi katika mazingira magumu Lilian Mbise wa kulia akipokea msaada wa mfuko wa mchele kutoka kwa mmoja wa wanawake wa kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi wakati wa halfa fupi iliyofanyika katika kituo hicho.
Baadhi ya watoto yatima na wale amabo wanaishi katika mazingira magumu katika kituo cha Sharom kilichopo kata ya Msangani wakiimba wimbo maalumu wakati wa halfa ya kukabidhiwa msaada wa vvyakula mbali mbali kutoka na kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi kwa lengo la kuwasaidia watoto hao waweze kupata mahitaji muhimu.
Mwenyekiti wa Kikundi cha PwaniGeneration Mwanamke sahihi Betty Msimbe akizungumza na watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu hawapo picha wakati wa sherehe hizo za kutoa msaada wa mahitaji mbali mbali ikiwemo vyakula.
Baadhi ya wanawake wanaounda kikundi cha Pwani Generationi mwanamke sahihi wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima mara baada ya sherehe za kukabidhi vyakula mbali mbali pamoja na mahitaji mengine ya msingvi katika kituo cha Sharom kilichopo kata ya Msangani Wilayani Kibaha.
Baadhi ya wanawake wa Kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi wakiwa wanawaangalia watoto hao yatima hawapo picha pindi walipokuwa wanaimba wimbo maalumu katika halfa hiyo ya kupatiwa msaada.
Mlezi wa wa kituo cha Sharom ambacho kinalelea watoto yatima pamoja na wale amabo wanaishi katika mazingira magumu akipiga makofi kwa furaha mara baaada ya kupokea msaada huo wa vyakula mbali mbali pamoja na mahitaji mengine kutoka kwa kikundi cha Pwani Generation mwanamke
Mlezi wa kulelea watoto yatima na wanaosihi katika
mazingira magumu Lilian Mbise akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na kituo hicho cha Sharaom kilipotembelewa na kikundi cha
Pwani Generation mwanamke sahihi pamoja na kutoa shukrani zake za
dhati kwa wanawake hao wa Mkoa wa Pwani kuweza kwenda kuwatembelea na
kuwafariji (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...