Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Salum Manyata  amewahasa wataalamu wa kutoa dawa za usingizi nchini kuwa wana jukumu kubwa la kuboresha utoaji wa huduma wa dawa za usingizi kwa kina mama wajawazito wakati wa upasuaji ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa utoaji huduma hiyo.

Dkt. Manyata ameyasema leo wakati akifungua mafunzo elekezi ya utoaji dawa za usingizi salama wakati wa upasuaji kwa kina mama wajawazito yanayofanyika jijini Mbeya kwa siku tatu na kushirikisha wataalamu kutoka vituo vya afya na hospitali zilizoko Nyanda Juu kusini.

Amesema kuwa ni vema washiriki hao kutumia fursa walioipata ya mafunzo hayo ya kujengewa uwezo ili kutekeleza yale ambayo wameyapata kwa kutoa huduma salama na sahihi.

Dkt. Manyata amewaasa wataalamu hao kupeleka mrejesho wa maswala mbailimbali mapya waliyoyapata kwa wengine katika vituo vyao watakaporejea ili kuhakikisha taratibu zote zinasimamiwa vizuri.

Mafunzo hayo yanatolewa na wakufunzi kutoka ndani na nje ya nchi na kushirikisha wataalam 35 wa dawa za usingizi kutoka Nyanda za Juu Kusini na kufadhiliwa na Chama cha Madaktari Bingwa  wa dawa za usingizi duniani (WFSA) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa  wa dawa za usingiizi Tanzania (SAFE) kwa malengo ya kuwajengea uwezo watoa huduma ya dawa ya usingizi katika vituo vya afya na hospitali vile vile kupunguza vifo vya kina mama wajawazito wakati wote wa upasuaji.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Salum Manyata  akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa  wataalamu wa kutoa dawa za usingizi wa vituo vya afya na hospitali Nyanda za juu Kusini katika ukumbi wa Usungilo jijini Mbeya
 Wataalam wa dawa za usingizi wakitoa elimu kuhusu namna ya kutoa huduma ya dawa za usingizi iliyo salama na sahihi kwa washitiri waliohudhuria mafunzo hayo.
 Baadhi ya washiriki vituo vya afya na hospitali wa nyanda za juu kusini wakifwatilia mada
 Wakufunzi Madaktari Bingwa wa Dawa za Usingizi katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Salum Manyata.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Salum Manyata  katika Picha ya pamoja na Viongozi Waratibu wa mafunzo ya huduma salama na sahihi ya dawa za usingizi na washitiri kutoka vituo vya Afya na Hospitali wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...