Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu na Utawala Bw. James Kibamba akizungumza na sehemu ya watumishi waliohudhulia mafunzo kuhusu namna sahihi ya kujinga na virusi vya ugonjwa wa Corona wakati akimkaribisha muwezeshaki Dkt. Peter Kibacha ambaye ni mtalaam bingwa wa afya na mtoto kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili. zoezi la kutoa elimu hiyo limefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali uliopo Jijini Dar es Salaam.
Bw. Yusuph Varisanga kutoka kitengo cha Uhasibu akiuliza sawali kuhusu ugonjwa wa Corona wakati zoezi la utoaji wa elimu kuhusu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo kiliendelea.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu Wa Serikali wakipata elimu kuhusu ugonjwa wa Virusi vya Corona, elimu hiyo imetolewa na mtaalam bingwa wa magonjwa ya afya na mtoto kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Peter Kibacha.

……………………………………………………………………………………………

Na. Dennis Buyekwa.

Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa hatari wa virusi vya Corona (COVID – 19). Muda wote wanapokuwa ndani na nje ya kituo cha kazi.

Wito huo umetolewa mapema leo ofisini hapo na Daktari bingwa wa magonjwa ya Afya na mtoto Dkt. Peter Kibacha kutoka Hosipitali ya Taifa Muhimbili wakati akitoa elimu juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

Kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Corona kiliibuka kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka jana katika mji wa Wuhan jimbo la Hubei nchini China, mpaka sasa umesambaa katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo nchi za Afrika Mashariki na hivyo kupelekea Shirika la Afya duniani (WHO) kuutangaza ugonjwa huo kuwa ni janga la dunia.

Dkt. Kibacha amesema ugonjwa wa Corona unaweza kumpata mtu yoyote hivyo amesisitiza kuwa ni vyema kuchukua tahadhari kila wakati hatua itakayosaidia watumishi hao kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa huo wao pamoja na familia zao.

Akizungumizia kuhusu dalili za ugonjwa huo Dkt. Kibacha amezitaja dalili hizo kuwa ni pamoja na mtu kupata homa kali, kukohoa kikohozi kikavu, uchovu wa mwili, kuharisha na kutapika, kupumua kwa shida sambamba na kukosa hamu ya chakula.

Akielezea kuhusu tiba ya ugonjwa huo Dkt. Kibacha amesema kuwa kwa sasa ugonjwa huo hauna chanjo wala tiba lakini kinachoweza kufanyika ni kufuata kanuni za afya ambazo zinaweza kuwasaidia watu kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Akiainisha njia za kujikinga na ugonjwa huo mtalaamu huyo amesema kuwa ni muhimu kwa kila mtu kujenga tabia ya kunawa mikono yake mara kwa mara pamoja na kujiepusha kugusana na mtu mwingine hasa pale watakapohitaji kusalimiana.

Amezitaja njia nyingine za kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo kuwa ni kuepuka kugusa macho, mdomo na pua kabla ya kunawa mikono, kuvaa barakoa wakati wote (Mask) pamoja kufunika kinywa kwa kitambaa kisafi wakati wote mtu anapokohoa au kupiga chafya.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu na Utawala Bw. James Kibamba amemshukuru mtaalamu huyo kwa kukubali wito wa kuja kutoa elimu hiyo kwa watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali huku akiwahimiza watumishi hao kutumia vyema elimu hiyo ili iweze kuwasaidia kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Nao watumishi waliopata mafunzo hayo wameushukuru uongozi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa kuandaa mpango wa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwa kuwa umewawezesha kupata elimu itakayowasaidia kujua njia bora za namna ya kujikinga na ugonjwa huo hatari unaosambaa kwa kasi duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...