Na Mwandishi wetu-NCAA
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.
Hamisi Kigwangalla ameshuhudia uvishwaji vyeo kwa menejimenti ya Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ikiwa ni utekelezaji wa sheria kwa taasisi
zilizoko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kujiendesha kijeshi katika
usimamizi wa Rasilimali za wanyamapori.
Katika sherehe hiyo wajumbe 15 wa
menejimenti ya Ngorongoro walivishwa vyeo ambapo idadi hiyo inajumuisha Naibu
Makamishna wa uhifadhi wawili na Makamishna wasaidizi Waandamizi wa uhifadhi
13.
Katika hafla hiyo Waziri Kigwangalla
ameielekeza menejimenti ya NCAA kutumia mafunzo mbalimbali ya kijeshi
waliyoyapata na kuhakikisha kuwa wanazingatia nidhamu ya kazi, kasi katika
utekelezaji wa majukumu na kuzingatia mtiririko mzuri wa amri hasa kwa
watumishi walioko chini yao ili kuhakikisha kuwaa utendaji kazi inaimarishwa na
kutatua changamoto ndogondogo kwa uharaka na kijeshi usu.
Mhe. Kigwangalla emesema kuwa sambamba na mafunzo mbalimbali ambayo
viongozi wa sekta za uhifadhi wamekuwa
wakiyapata katika vyuo vya jeshi usu vya Mlele na Mbulumbulu wizara yake itashirikiana
na Jeshi la Polisi ili kuwapa kozi ya uongozi wa masuala ya kijeshi katika chuo
cha Polisi Moshi ili kuongeza ufanishi wa usimamizi wa mifumo ya kijeshi katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro Profesa Abihudi Kaswamilla amemhakikishia Waziri Kigwangalla
kuwa, bodi anayoiongoza itaendelea
kusimamia utekelezaji wa mfumo wa jeshi usu kwa watendaji wa NCAA ili
kuhakikisha kuwa majukumu makuu ya uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii
yanatekelezwa ipasavyo.
Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Dkt.
Freddy Manongi amebainisha kuwa Mamlaka hiyo itaendelea kusimamia uteekelezaji
wa mfumo wa jeshi usu kwa watumishi wa Mamlaka hiyo ili kuhakikisha kuwa sekta
ya utalii inayochangia fedha za kigeni kwa asilimia 25 na pato la taifa kwa
zaidi ya asilimia 17 inazidi kuimarika na kuongezeka.
Viongozi wengine waliohudhuria hafla
hiyo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mhe. Mrisho Gambo, wakuu wa Wilaya za Ngorongoro na Karatu, Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini IGP Saimon Sirro, Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA Dkt Allan Kijazi na viongozi wengine
kutoka vyombo vya ulinzi na Usalama.
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Prof. Abihudi Kaswamila (aliyevaa suti) akimvalisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia utawala na Rasilimali watu Bw. Samson Ntunga.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla akiongea na watendaji pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro baada ya hafla ya uvishwaji Menejimenti ya Mamlaka hiyo.
Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Dkt Freddy Manongi akitoa taarifa kwa Waziri wa Maliasili na utalii Dkt Hamis Kigwangalla ( hayupo pichani) kuhusu utekelezaji wa sheria ya jeshi Usu katika utendaji kazi wa Mamlaka hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...