Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Marubani na wahudumu wa
Shirika la Ndege la Tanzania
(ATC) kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere
kuelekea Tanga , Machi 1, 2020. Waziri mkuu ameanza ziara ya kikazi ya
Mkoa wa Tanga kwa kutekeleza maelekezo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) aliyoyatoa kwa
Watanzania ya kutosalimiana kwa kushikana mikono au kukumbatiana ikiwa
ni tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (wa pili
kushoto) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu wakati
alipoowasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga,Machi 1, 2020. Waziri mkuu ameanza ziara ya kikazi ya Mkoa wa Tanga kwa kutekeleza maelekezo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) aliyoyatoa kwa Watanzania ya kutosalimiana kwa kushikana mikono au kukumbatiana ikiwa ni tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...