Na Luteni Selemani Semunyu
Waziri wa Habari utamaduni sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe
amesema Serikali itahakikisha inatafuta ufumbuzi wa changamoto wa
Uhaba na Ubovu wa viwanja Vya Mchezo wa Golf hapa Nchini na kuliomba
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kusaidia kukabiliana na
Changamoto hiyo
Wazirii Mwakyembe alisema hayo jana wakati akifunga mashindano ya
mchezo wa gofu ya TANAPA Lugalo Open yaliyofanyika katika Viwanja vya
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania vya Lugalo Jijini Dar es
Salaam.
Waziri Mwakyembe alisema mchezo wa gofu umekua na changamoto nyingi
hasa ya ubovu na uchache wa miundombinu ya viwanja hivyo serikali
itahakikisha changamoto hizo zinatafutiwa ufumbuzi kwa kushirikiana na
wadau wa sekta ya michezo.
“Natoa rai kwa wadau mbalimbali wa michezo kuwekeza kwenye mchezo wa
gofu ili kuuendeleza mchezo huo nalipongeza Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania imekuwa Chachu yaa Kuendleza Mchezo huu na kuvipa
nguvu Vyma vya Golf kwa Kuwapa Ofisi “ Alisema Dk Mwakyembe.
Pia Waziri Mwakyembe ametoa wito kwa wadhamini wakuu wa mashindano
hayo ambao ni Tanapa kuendelea kudhamini mchezo wa kwani mchezo huo
unanafasi kubwa katika kuutangaza utalii wa nchi na Taifa kwa Ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo Brigedia Jeneral
Mstaafu Michael Luwongo amemuomba Waziri Mwakyembe kupitia wizara yake
kuupa kipaumbele na kuutangaza mchezo wa gofu ili Tanzania itambulike
kimataifa kupitia mchezo wa huo kutokana na michezo mingi hapa nchini
kutangazwa zaidi.
Nae Mwakilishi wa TANAPA Hassan Ngulume ambao wamedhamini mashindano
hayo alisema wameshukuru kwa kupata nafasi ya kudhamini Golf na
kuahidi kuendelea kutoa udhamini ili kuongeza uelewa wa hifadhi kwa
watalii hasa wa ndani.
Kwa upande wa matokeo ya mashindano hayo mchezaji Victor Joseph wa
klabu ya Dar es salaam gymkhana ameibuka na ushindi baada ya kupiga
mikwaju 153 wakati mshindi wa jumla aliyepiga Mikwaju ya Jumla Net 142
ni Godfrey Abel.
Wakati Katika Divisheni B Mshindi ni Fabian Magoti aliyepiga mikwaju
ya Jumla 143 huku Mshindi wa Pili ni Zakaria Edward aliyepiga mikwaju
ya Jumla 148 wakati Divisheni B Mshindi ni John Hiza wa Lugalo kwa
Mikwaju ya Jumla 143 akifuatiwa na Teddy kalinga kwa Mikwaju ya Jumla
145.
Divisheni C Mshindi ni Nathaniel Ayonga wa Lugalo Kwa Mikwaju ya
Jumla 148 akifuatiwa na Laurent Sangawe naye wa Lugalo kwa Net ya 150
huku kwa Wanawake Mshindi ni Angel Eaton kwa mikwaju 159 bada ya
kufungana mshindi kwa wanawake kwa mikwaju ya jumla 147 ni Hawa
Wanyenche.
Mshindi wa wa pili kwa wanawake kwa mikwaju ya jumla 151 ni Ayne
Magombe wakati mshindi kwa wazee ni Jin Soo Yang aliyepiga mikwaju
ya jumla 151 na kufuatiwa na Dk Edmund Mdolwa aliyepiga mikwaju ya
jumla 152
Kwa upande wa watoto mshindi kwa kwanza ni Karim Ismail aliyepiga
Mikwaju ya jumla 69 akifuatiwa na Hamad Maulid aliyepiga mikwaju ya
jumla 70.
Washindi
Washindi wa Shindano la Tanapa Lugalo Open kwa mwaka 2020 wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa habari Utaamaduni sanaa na Michezo DkHarisson Mwakyembe na baadhi ya Viongozi wa Golf mara baada ya kupatiwa zawadi zao katika Hfla iliyofanyika jana Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Jumla wa mashindano ya Tanapa Lugalo Open kwa mwaka 2020 akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa habari Utaamaduni sanaa na Michezo Dk Harisson Mwakyembe na viongozi wengine wa Golf mara baada ya kupatiwa zawadi zao katika Hfla iliyofanyika jana Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Mshindi kwa Wanawake Hawa Wanyenche akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Gofu Tanzania Anita Siwale wakati wa ufungaji mashindano ya Tanapa Lugalo Open kwa mwaka 2020 katika Hafla iliyofanyika jana Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Mshindi kwa wazee Wanawake Stephania Sayore akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Michezo Jeshini Meja Penina Igwe wakati wa ufungaji mashindano ya Tanapa Lugalo Open kwa mwaka 2020 katika Hafla iliyofanyika jana Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Mshindi kwa Watoto Karim Ismail akipokea zawadi ya baiskeli kutoka kwa
moja ya wadhamini Brenda Dickson wakati wa ufungaji mashindano ya
Tanapa Lugalo Open kwa mwaka 2020 katika Hafla iliyofanyika jana
Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...