Na Khadija
Khamis –Maelezo Zanzibar
Wizara ya
Afya Zanzibar imepokea msaada wa vifaa
mbali mbali vya afya kutoka kwa Mdau wa
Maendeleo Said Nassir Nassor Bopar kwa ajili ya kupambana na kujikinga na
maambukizi ya Corona.
Akipokea
msaada huo Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed huko katika Wizara ya Afya Mnazi
mmoja amesema vifaa hivyo vitasaidia kutoa huduma mbali mbali za matibabu
pamoja na kupambana na ugonjwa wa corona nchini.
Vifaa
vilivyotolewa ni pamoja na vitanda 36, mashuka, sanitizer, friji la kuhifadhia
damu, mashuka, mask, mito na kiti cha kubebea wagojwa ambavyo vitasaidia kutoa
huduma na kujikinga maambukizi ya corona.
Amesema
serikali inahitaji vifaa vingi kutokana na kuwepo kwa wagonjwa ambao wanahitaji
kupatiwa matibabu na wananchi kujikinga maambukizi ili yasienee nchini
“Mdau huyu
wa maendeleo ameleta vifaa hivi wakati mzuri kwa kuangalia shida iliopo hivi
sasa kutokana na kufunguliwa kituo kipya cha kidimni ambacho kinahitaji vifaa
mbali mbali kwa wagonjwa waliopata maambukizi ya Corona”, alifahamisha Waziri
Hamad.
Aidha Waziri
wa Afya amemshukuru Mfanyabiashara huyo kwa msaada huo ambao utasaidia kutoa
huduma mbali mbali kwa wagonjwa na kupunguza maambukizi pamoja kuweza kupambana na kupiga vita
ugonjwa wa Corona.
Hata hivyo
Waziri huyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari za mapema kwa kuepuka
mikusanyiko na kufuata maagizo yanayotolewa na serikali ili kujikinga na
maambukizi ya Corona.
“Wananchi
wasikae vikundi vikundi wabakie Majumbani mwao na kuwadhibiti watoto wao
kufanya hivyo kutasaidia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona
nchini”, alisema Waziri wa Afya .
Ameitahadharisha
jamii kuchukua tahadhari ya kukaa umbali wa mita moja na kufuata maadili na
masharti ya wataalamu wa afya kufanya hivyo kutasaidia kuepusha ongezeko la
maambukizi kwa kufanya hivyo kutapunguza
kusambaa kwa maambukizi hayo.
Alisisitiza
kuwa wananchi ambao wana wagonjwa katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja kupanga
utaratibu wa kuwahudumia wagonjwa wao kuingia
watu wawili tu ili kuepusha msongamano mkubwa ambao utahatarisha maisha
yao kwa kupata maambukizi mapya ya Corona .
Nae Mdau wa
Maendeleo ambae ni Mfanyabiashara Maarufu Said Nassir Nassor Bopar alisema ametoa msaada huo kwa lengo la
kuokoa maisha ya jamii kutokana na hali halisi iliyopo ya mripuko wa maradhi ya
corona pamoja na kujikinga maambukizo
hayo.
Alieleza
kuwa ataendelea kuisaidia serikali kila hali inaporuhusu ili kuweza kutoa
huduma bora kwa wananchi pia anatarajia kutoa msaada mwengine katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya
Kaskazini A pamoja na Kisiwani Pemba .
“Kila
panapotokea tatizo kupenda kuisaidia jamii ili kuepukana na athari ambazo
zitaweza kujitokeza tuweze kuzikabili kwa namna moja au nyengine kwa wakati
muafaka “alisema Bopa.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed (kulia)akikabidhiwa Vifaa
mbalimbali na Mfanya Biashara Said Nassir Nasor (BOPER)kusaidia wenye
maradhi mbalimbali ikiwa pamoja na Korona miongoni mwa Vifaa hivyo ni
Vitanda ,Mashuka Sabuni za Kunawa mikono , Viti vya Walemavi na Dawa
mbalimbali hapo Wizara ya Afya Zanzibar. 
Vifaa mbalimbali vikitolewa na mfanya biashara Said Nassir Nasor (BOPAR
)wa kwanza kushoto kwa ajili ya kusaidia wenye maradhi mbalimbali ikiwa
pamoja na Korona miongoni mwa Vifaa hivyo ni Vitanda ,Mashuka Sabuni za
Kunawa mikono , Viti vya Walemavi na Dawa mbalimbali hapo Wizara ya
Afya Zanzibar.
Vifaa mbalimbali vikitolewa na mfanya biashara Said Nassir
Nasor(BOPAR )kwa ajili ya kusaidia wenye maradhi mbalimbali ikiwa
pamoja na Korona miongoni mwa Vifaa hivyo ni Vitanda ,Mashuka Sabuni za
Kunawa mikono , Viti vya Walemavu na Dawa mbalimbali hapo Wizara ya Afya
Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Waandishi wa
Habari katika Hafla ya kukabidhi Vifaa mbalimbali
kusaidia wenye maradhi mbalimbali ikiwa pamoja na Korona miongoni mwa
Vifaa hivyo ni Vitanda ,Mashuka Sabuni za Kunawa mikono , Viti vya
Walemavi na Dawa mbalimbali hapo Wizara ya Afya Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...