Wadau wakiendelea kupata mafunzo kutoka kwa watoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa Shirika la Internet Society Tanzania Chapter (ISOC) Pamela Chogo akijibu maswali ya wadau wa mtandao wakati wa mafunzo hayo.
 Baadhi ya wadau wa masuala ya mtandao wakiwa kwenye semina ya mafunzo ya usalama kwa watumiaji wa intaneti yaliyoandaliwa na Shirika la Internet Society Tanzania Chapter(ISOC)leo Machi 14 mwaka 2020.Mafunzo hayo yamefanyika wilayani kigamboni jijini Dar es Salaam.
Wadau wa mtandao wakiwa makini kufuatilia mambo mbalimbali kwenye simu zao za mkononi kabla ya kuanza majibu maswali mbalimbaliambayo wametakiwa kuyajibu baada ya kupata mafunzo ya matumizi sahihi ya mtandao.
Sehemu ya wadau wakiendelea kujadiliana wakati wa mafunzo ya matumizi sahihi ya mtandao pamoja na usalama wake kwa mtumiaji.
Katibu Mkuu wa Shirika la Internet Society Tanzania Chapter (ISOC) Pamela Chogo akitoa mada kwa wadau wa mtandao wakati wa mafunzo yaliyokuwa yanahusu umuhimu wa kuzingatia usalama kwa watumiaji wa intaneti.


Rais wa Shirika la la Internet Society Tanzania Chapter (ISOC) Nazarius Nicholas (aliyeshika simu) akifafanua jambo wakati wa utoaji mafunzo kwa wadau na watumiaji wa mtandao.
Baadhi ya wadau wa mtandao wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali ambazo zilikuwa zinatolewa kwenye mafunzo hayo kutoka kwa watalaam wa masuala ya mtandao nchini.


Watumishi wa Shirika la Internet Society Tanzania Chapter wakifuatilia jambo kwenye simu ya mkono wakati wa mafunzo hayo yakiendelea.



Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

KATIBU wa Shirika la Inrenet Society Tanzania Chapter(ISOC) Pamela Chogo amesema kuna kundi kubwa la watumiaji wa simu za mkononi ambazo wamezinunua kwa gharama kubwa lakini matumizi yake hayaendani na gharama hizo.

Ameyasema hayo leo wakati akitoa mada katika mafunzo ya matumizi salama ya mtandao yaliyoandaliwa na Shirika hilo kwa wadau wa mtandao wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo amefafanua katika simu za mkononi kuna kila kitu lakini watumiaji wengi hawajaweza kuzitumia ipasavyo.

Ametoa mfano kuna waliotumia fedha nyingi kwa ajili ya kununua simu lakini matumizi yake hayana tofauti na mwenye simu ya tochi."Unaweza kukuta mtu ameunua simu ya Sh.milioni moja au mbili lakini matumizi yake hayaendani na thamani halisi ya simu hiyo.

"Kwenye simu kuna kila kitu ambacho kinaweza kumsaidia mwenye nayo kufanya mambo makubwa ya maendeleo na hata kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kila siku."

Amefafanua watumiaji wengi wa simu wanazitumia kwa matumizi ya kawaida ikiwemo kupiga na kupokea simu, kutuma na kupokea ujumbe na kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii, hivyo ameshauri umefika wakati wa kutumia simu kwa matumizi sahihi na salama kwa maendeleo ya mtumiaji na Taifa kwa ujumla.

Akizungumzia matumizi sahihi kuhusu intaneti, Chogo amesema kuna kila sababu ya mtumiaji wa intaneti kuwa makini na paswadi yake kwa kuhakikisha inakuwa ya kwake tu badala ya kumpa mtu mwingine kwani madhara yake ni makubwa yakiwemo ya taarifa zake kuchukuliwa na kutumika kinyume na malengo ya mhusika.

Ametoa rai kwa watumiaji wa mtandao kuhakikisha paswad (nywila) ibaki kuwa siri ya mtu husika na hiyo itasaida taarifa na matumizi ta intanet kuwa salama.

Pia amesema kwa watumiaji wa mtandao hakuna sababu ya kila ujumbe ambao unatumiwa kwenye simu yako kutuma kwa wengine."Hakuna sababu ya kila unachotumiwa kwenye simu na wewe uka foward kwa mwingine."

Wakati huo huo Chogo amesema ni wajibu wa watumiaji wa mtandao kuwa makini na kila wanachotuma na kuweka kwani unapoweka kitu mtandaoni kinaishi na hivyo ni muhimu kuiangalia zaidi kesho yako kwani hata ukifuta bado kinabaki mtandaoni.

“Tutumie data za simu hizi kwa ajili ya kutuingizia pesa zaidi badala ya matumizi ya kawaida ambayo hayana tija kubwa kwetu. Unakuta mtu amenunua simu ya sh milioni mbili lakini matumizi yake hayazidi asilimia 20 ya pesa hiyo. Simu zetu zina mambo mengi lakini hatuzitumii ipasavyo,"amesema.

Kwa upande wake, Rais wa ISOC -Tanzania, Nazarius Nicholas ametumia semina hiyo kuwataka wananchi kutumia teknolojia na hasa iliyopo katika mtandao kwa maendeleo ya Taifa.

Amesema moja ya mambo ambayo Shirika hilo inayahimiza ni matumizi sahihi ya mtandao kwani kuna baadhi ya watumiaji wamekuwa wakiitumia ndivyo sivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...