Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkurugenzi
wa Lebo ya Kings Music Records Ali Saleh Kiba amewataka mashabiki wa
muziki kukaa tayari kumpokea msanii wake mpya Tommy Flavour.
Ni
takribani siku tatu zimepita toka msanii huyo kupoteza wasanii wake
wawili Cheedy na Killy tz walioamua kuondoka kwenye lebo ya Kings Music
Records.
Akiandika katika
mtandao wake wa Kijamii, Ali Kiba amesema kuwa Ijumaa hii
atamtambulisha msanii mpya chini ya lebo ya Kings Music Records na
kuwataka mashabiki wake wajiandae kumpokea.
"It’s
official kwamba this Friday @kingsmusicrecords inamtambulisha rasmi
@tommyflavour kwenye music industry. Kuwa wa kwanza kusikiliza na
kuangalia kazi zake mpya kwa subscribe kwenye Youtube Channel ya Tommy
Flavour"
Mbali na hilo,
Ali Kiba anatarajia kuwa msanii wa pili kufanya tamasha la Live
wakiliita Hima TVE Chill and Feel the Vibe kupitia kituo cha Luninga cha
ETV ambao ataimba na kuwaburudisha mashabiki wake wakiwa nyumbani.
Ali
Kiba kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa Dodo unaofanya vizuri
kwenye mitandao mbalimbali akiwa amemshirikisha msanii na mwanamitindo
Hamisa Mobeto kama Video Vixen.
Msanii
wa kwanza kufanya tamasha la Live alikua ni Nandy na aliweza kuvalishwa
pete ya Uchumba na rafiki yake wa siku nyingi msanii mwenzake Billinas.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...