Na Ripota Wetu,Michuzi TV

SIKU moja baada ya msanii marufu nchini Nassib Abdull a.k.a Diamond Platnumz kutangaza kuchangia Kodi ya pango kwa kaya 500 nchini ,Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara ameamu kivunja ukimya huku akimtaka aoe ili wakakutane peponi.

Diamond kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ametangaza kusaidia kuchangia kod kwa kaya hizo 500 na utaratibu kwa watakaochangiwa utatolewa kesho Jumatatu ya Aprili 27 mwaka huu.

Baada ya ujumbe huo ,Manara ameamua kumpongeza Diamond kwa kuamua kuchangia Kodi ya pango.Manara kupitia mtandao wake wa kijamii ameandika hivi"Sijawahi kujuta kuwa na ushkaji na wewe.Wapo wabishi watasema mbona umetangaza ...ahhh hii ni kwa ajili ya kuinspire wengine waliojaaliwa kidogo kuwatazama wenzao.

" Unajua nini mwamba , Mungu atakuongezea ile mbaya...atakufungulia riziki zaidi na kwa sasa bado kitu kimoja ukifanya hivyo na peponi tutakaa wote In shallah...OA."

Hata hivyo baada ya ujumbe huo Diamond naye akaamua kumjibu Haji Manara kwa kumwambia kuwa " Ni kweli Mkuu na sisi masikini ndio tunapaswa kuwa mstari wa mbele kwenye kusaidiana maana uchungu wake tunaujua zaidi.

Kwa kukumbusha tu, Diamond ameamua kusaidia kaya hizo baada ya kuona changamoto ambazo Watanzania wanazipitia kwenye kipindi hiki cha janga la Corona ambapo kwa sehemu kubwa shughuli za kiuchumi zimeyumba na yeye ni miongoni mwa miongoni mwa walio ndani ya janga hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...