Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewatahadharisha Wananchi kuzingatia kwamba Karantini wanaowekewa Watu walioingia Nchini kutoka Nje ya Nchi sio adhabu  bali ni utaratibu unaozingatia Muongozo wa Wataalamu wa Afya katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona vinavyosababisha Mafua na Homa Kali ya Mapafu.

Balozi Seif Ali Iddi ametoa tahadhari hiyo huko Nyumbani Kwake Mtaa wa Kama Kaskazini Kidogo ya Mji wa Zanzibar  wakati akitoa Taarifa kwa Umma baada ya kumaliza muda wake wa wa mapumziko ya Siku 14 zinazomuwajibika Kila Msafiri aliyeingia Nchini kutoka nje ya Nchi kwa mujibu wa Wataalamu.

Hata hivyo Balozi Sif alisema kwa mujibu wa Wataalamu wa Sekta ya Afya walimshauri aendelee kuongeza Siku Saba Zaidi ili kumaliza vyema Karantini hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Mawaziri wa Afya wa Serikali ya Muungano waTanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada wanazoendelea kuzichukuwa katika kuipatia Jamii Taarifa sahihi juu ya muenendo mzima wa Virusi vya Corona.

Imetolew na Kitengo cha Habari (OMPR)
April 02, 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...