Mlipuko wa homa kali ya mapafu, COVID-19 au Virus via
Corona, umeleta athari katika nyanja mbalimbali za kiuchumi kote duniani,
ikiwemo sekta ya ajira. Baadhi ya makampuni yamelazimika kupunguza idadi ya
waajiriwa, mengine yakilazimika kufunga biashara na uzalishaji, huku mengine
yakisaidia juhudi za seriali na hata sekta binafsi kukabiliana na matokeo ya
mlipuko wa virusi vya Corona ili kusaidia kurudisha mataifa katika kawaida ya
uzalishaji.
Hapa Tanzania, makampuni Mengi yamechangia rasilimali katika
juhudi za serikali na za taasisi za tiba kwenye kukabiliana na maradhi hayo.
Vilevile, mkampuni mengi ya ajira, ikiwemo BrighterMonday Tanzania, kampuni
kubwa zaidi inayojihusisha na ajira na rasilimali watu, imechukua hatua
kuangazia changamoto za udhibiti rasilimali watu pamoja na changamoto
zinazowakabili waajiri nchini Tanzania.
Katika utafiti wao, BrighterMonday imewahoji maafisa
rasilimali watu kutoka sekta mbalimbali za ajira nchini na kuwauliza changamoto
wanazokutana nazo katika kuajiri hasa wakati huu wa mlipuko wa virusi vya
corona. Maofisa hao wameeleza kuwa wanapitia wakati mgumu kupata watu wenye
vigezo vinavyohitajika kwa ajili ya kuwaajiri bila kuonana nao ana kwa ana kwa
ajili ya usaili. Changamoto hii ndiyo iliyofanya kampuni ya BrighterMonday
kubuni njia mbadala ya kusuluhisha tatizo hilo.
Akizungumzia hili, Mkurugenzi wa BrighterMonday Tanzania,
Reshma Bharmal-Sharriff amesema kuwa
wanaelewa changamoto zinazowakabili kibiashara na chagamoto za maafisa
rasilimali watu nchini.
"Kwa kulitambua hili, tunatoa ofa ya matangazo ya kazi
kwa wateja wetu wote kwa muda wa miezi mitatu kuanzia mwezi huu wa Aprili hadi
June ili kuhakikisha kuwa waajiri wanafanya kazi zao katika mazingira
mazuri," amesema Reshma, huku akiongeza kuwa kampuni yake imejipanga
kujitoa kuwasaidia wale wote walio katika mstari wa mbele kupambana na
maambukizi ya virusi vya corona kwa kutoa punguzo kwa baadhi ya huduma za ajira.
"Lengo letu ni kuhakikisha kuwa waajiri wanakuwa na watu sahihi
wanaowahitaji kwa ajili ya kazi zao."
Reshma ameongeza kuwa kampuni yake inahakikisha kuwa wakati
huu wa mlipuko wa virusi vya corona mchakato wa kuajiri unakuwa mzuri na wenye
faida. "Kwa kutumia mfumo wa Uainishaji wa Ujuzi wa BrighterMonday,
tunataka kuhakikisha kuwa waajiri wanaridhika na mfumo wa usahili na waajiriwa
watakaopatikana watakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi kama walivyoainisha
katika vyeti vyao, amesema Reshma.
Bi. Reshma anaeleza kuwa kampuni yao imeandaa mfumo wa
uchakataji wa taarifa za mwombaji ambao unaweza kumsaidia mwajiri kuchambua
sifa kadhaa za mwombaji, ikiwemo kiwango cha elimu na ujuzi alionao. Hii
inamwezesha mwajiri kuweza kulinganisha kwa urahisi vigezo anavyohitaji ili
kumpata mtu sahihi atakayemwajiri kwa muda mfupi na kwa umahiri mkubwa.
Kampuni hiyo imejipanga kuwasaidia waajiri kuchambua na
kupata waombaji watakaofaa kwa kazi wanazohitaji bila kujali hali ya kiuchumi
inayoikabili dunia kwa sasa. Hivyo, kama unahitaji kupata wafanyakazi bora
wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona, unaweza kufanya hivyo kwa urahisi.
Mkurugenzi wa BrighterMonday Tanzania,
Reshma Bharmal-Sharriff
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...