Na Amiri kilagalila,Njombe
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameagiza kila mwananchi kuhakikisha anapambana na virusi vya Corona (COVID-19) kwa hiari ili taifa liweze kubaki salama.
Msafiri ametoa agizo hilo mapema alfajiri ya leo April 22 2020 wakati akiongoza zoezi la utakasaji mabasi yanayoelekea mikoa mingine kutokea kituo cha mabasi Njombe mjini kwa Croline,zoezi ambalo limeratibiwa na halmashauri ya mji wa Njombe.
“Kila mwananchi ajione ni mdau katika zoezi la kupambana na virusi hawa na kuhakikisha hawafiki kwetu,na kila mmoja awe tayari kushiriki zoezi hili kwa hali na kwa hiari kama tulivyopambana vita vya Kagera ili taifa letu libaki salama”alisema Ruth Msafiri
Aidha ametoa wito kwa halmashauri ya mji wa Njombe kuweka utaratibu endelevu wa upuliziaji dawa magari katika stendi hiyo huku akipongeza uongozi wa halmashauri hiyo kwa kujitoa na kutafuta vitakasa magari kwa ghalama naafuu.
“Nichukue nafasi kwa kuipongeza halmashauri ya mji wa Njombe kwa kujiongeza yenyewe na kuona inaweza ikajaribu kufanya zoeze hili,tutaliwekea utaratibu mzuri liwe endelevu na ninampongeza mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe pamoja na wafamasia wake walivyobuni ule utaraibu wa kitaalam wakitupatia vitakasa magari ambavyo vina ghalama naafuu”alisema tena Ruth Msafiri
Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe Dkt,Isaya Mwasubila amesema swala hilo la upuliziaji dawa ni nyongeza katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona na litaendelea sambamba na njia nyingine ili kuhakikisha mji wa Njombe unakuwa salama.
“Zoezi tulilofanya lina tija kubwa lakini sawala hili la upulizaji litakwenda pamoja na mikakati yote kuleta tija kwa asilimia mia moja kwa hiyo si swala la kunawa mikono peke yake ila ni kwa ujumla wake ili wananchi wetu wajue namna ya kujikinga na kuhakikisha mji wetu wa Njombe unakuwa salama”alisema Mwasubila
Petro Ndendya ni mmoja wa madereva wa mabasi ya safari ndefu ambaye basi lake limeweza kunyunyiziwa dawa,amepongeza halmashauri ya mji wa Njombe kwa hatua hiyo kwa kuwa magari yao yamekuwa yakibeba abaria wa aina tofauti.
“Kwa kweli naipongeza serikali kwa kitendo hiki kwa kuwa abiria wengi wanarudi huku Njombe na hatujui kama wameathirika au hapana,pia ninashauri juhudi hizi ziendelee maambukizi haya yatakapofika mwisho”alisema Ndendya
Kelvin Mwalwanda ni mwenyekiti wa stendi ya mkoa wa Njombe (mji Njombe),amesema ataendelea kuhakikisha anahamasisha zoezi la kufuata taratibu zote za kujikinga na virusi hivyo katika stendi ya Njombe.
“Nitahakikisha ninaendelea kuhamasisha zoezi la kujikinga na Corona linakuwa endelevu na kuhakikisha kila abaria ana nawa mikono kwa kuwa unapojikinga wewe maana yake unamkinga mwingine”alisema Kelvin Mwalanda Serikali nchini Tanzania inaendelea na juhudi mbali mbali za kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19) lakini hata hivyo licha jitihada ambazo zinaendelea hii leo Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Majaliwa Kasim Majaliwa ametangaza ongezeko la visa vya Corona na kufikia 284 kutoka 254 vilivyotangazwa awali na wizara ya afya huku kati ya hao wagonjwa 256 wakiendelea vizuri,wagonjwa 7 wakiwa kwenye uangalizi wa karibu huku kadhalika wagonjwa 11 wakiwa wamepona kabisa.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...