Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
LICHA
ya Shirika la Afya Duniani kusema wazi kuwa pombe haiwezi kupigana
dhidi ya virusi vya Corona (Covid-19) na kuwashauri watu wapunguze
matumizi yake Gavana wa Mji mkuu wa Nairobi, nchini Kenya Mike Sonko
kupitia mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika mapema jumanne valithibitisha
matumizi ya pombe katika Kupambana na virusi hivyo kwa kile alichoeleza
kuwa pombe aina ya Hennessy ni kitakasa koo "throat sanitizer." CNN
imeripoti.
Sonko
aliwasilisha mpango huo mbele ya waandishi wa habari na kutangaza azma
yake ya kuambatanisha chupa ndogo za pombe aina ya Hennessy katika
vifurushi vya chakula vitakavyotolewa kwa familia duni wakati wa kipindi
hiki cha mlipuko wa virusi vya Corona.
Imeelezwa
kuwa Gavana huyo alihalalisha kuingizwa kwa pombe katika vifurushi vya
kujikinga na kuenea kwa virusi hiyo ikiwa kama kitakasa koo.
"Nadhani
kutokana na utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Ulimwenguni na
mashirika anuwai, inaaminika kwamba pombe inachukua jukumu kubwa katika
kuua virusi vya Corona." Sonko alieleza kwenye video.
"Tutakuwa
na chupa ndogo za Hennessy kwenye pakiti za chakula ambazo tutakuwa
tukiwapa watu wetu ..." Alieleza Gavana huyo wa Nairobi Mike Sonko.
Ikumbukwe
kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) imeonya kwamba kunywa pombe si kinga
dhidi ya COVID-19 na inaweza kuwa hatari zaidi na likaweka wazi kuwa
pombe hailindi dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona, na kuwashauri watu
kupunguza matumizi yake.
Katika
chapisho lililotolewa na shirika la Afya duniani (WHO) siku ya Jumanne
lilisema kwamba pombe inaweza kudhoofisha afya ya mtu na kufanya wawe
katika hatari kubwa ya virusi ikiwa ni pamoja na Covid-19.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Amref Health Africa Githinji Gitahi ameeleza kuwa pombe ni
faida isiyo ya faida ya matibabu, katika chapisho lake kupitia ukurasa
wa Twitter alilaani madai ya Sonko na aliwataka Wakenya waondoe pombe
hiyo.
Hii sio mara ya
kwanza Sonko kukutana na uchunguzi wa madai, Gavana huyo alikamatwa
mwishoni mwa mwaka jana kwa tuhuma za ufisadi ambazo alizikana na
kulazimika kukabidhi majukumu yake kadhaa kwa serikali ya kitaifa.
Wakati
huo huo, kampuni ya vinywaji ya Hennessy kupitia vyombo vya habari
imepinga madai ya Gavana huyo ya kwamba kunywa au kutumia pombe
kunaweza kuzuia virusi vya Corona.
"Hennessy
inapenda kusisitiza kwamba unywaji wa chapa yetu au kileo kingine
chochote cha pombe hailindi dhidi ya virusi," ilieleza sehemu ya
taarifa yake kupitia News News ya Nairobi.
Imeelezwa kuwa CNN haikuweza kufikia Sonko kwa maoni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...