Mtalaam wa Afya akipuliza dawa
katika gari linalofanya safari zake kutoka Bariadi Mkoani Simiyukwenda
jijini Dar es Salaam leo Aprili 17, 2020 wakati wa kuhamasisha zoezi
endelevu la upuliziaji dawa katika magari ya abiria ambalo limekuwa
likifanyika katika kituo cha Mabasi cha Somanda Mjini Bariadi na Vituo
vingine ikiwa ni moja ya jitihada za kupambana na maambukizi ya Virusi
vya Corona.

Mtalaam wa Afya akipuliza dawa
katika gari linalofanya safari zake kutoka Bariadi Mkoani Simiyu kwenda
jijini Dar es Salaam leo Aprili 17, 2020 wakati wa kuhamasisha zoezi
endelevu la upuliziaji dawa katika magari ya abiria ambalo limekuwa
likifanyika katika kituo cha Mabasi cha Somanda Mjini Bariadi Vituo
vingine ikiwa ni moja ya jitihada za kupambana na maambukizi ya
Virusi vya Corona.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Dkt. Festo Dugange(kulia) akionesha maji yaliyochanganywa na dawa
ambayo yatatumika kuwanawisha wasafiri watakaopanda magari ya abiria
katika vituo mbalimbali baada ya magari kupuliziwa dawa mwanzo wa
safari, wakati wa kuhamasisha zoezi endelevu la upuliziaji dawa katika
magari ya abiria ambalo limekuwa likifanyika katika kituo cha Mabasi cha
Somanda Mjini Bariadi na Vituo vingine ikiwa ni moja ya jitihada za
kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Dkt. Festo Dugange akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa
Simiyu kabla ya wakati wa uzinduzi wa zoezi endelevu la upuliziaji dawa
katika magari ya abiria ambalo limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka katika kituo cha Mabasi cha Somanda Mjini Bariadi
ikiwa ni moja ya jitihada za kupambana na maambukizi ya Virusi vya
Corona.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wananchi na viongozi wa Mkoa wa
Simiyu, wakati wa kuhamasisha zoezi endelevu la upuliziaji dawa katika
magari ya abiria ambalo limekuwa likifanyika katika kituo cha Mabasi cha
Somanda Mjini Bariadi na Vituo vingine ikiwa ni moja ya jitihada za
kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

-Mtaalam wa Afya wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi, Marko Igenge akipuliza dawa katika gari linalofanya
safari zake kutoka Bariadi Mkoani Simiyukwenda jijini Dar es Salaam leo
Aprili 17, 2020 wakati wa kuhamasisha zoezi endelevu la upuliziaji dawa
katika magari ya abiria ambalo limekuwa likifanyika katika kituo cha
Mabasi cha Somanda Mjini Bariadi na Vituo vingine ikiwa ni moja ya
jitihada za kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona.
*************************************
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amesema Simiyu itaendelea kufuata maelekezo ya Serikali
katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona, ikiwa ni
pamoja na kuwatowaweka karantini wasafiri wanaotoka katika mikoa yenye
maambukizi kama inavyopendekezwa na baadhi ya wananchi badala yake
itawaweka wasafiri kutoka nje ya nchi.
Mtaka ameyasema hayo leo Aprili
17, 2020 wakati wa uhamasishaji wa zoezi endelevu la upuliziaji dawa
kwenye magari ya abiria katika kituo kikuu cha mabasi Bariadi, ikiwa ni
sehemu ya jitihada za kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona,
ambalo limeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
“Tumeona kauli za viongozi
mbalimbali, tumeona pia jumbe za watu wa Simiyu katika mitandao
mbalimbali ya kijaamii ambao wangetamani watu kutoka katika mikoa yenye
maambukizi wawekwe karantini sisi kama mkoa tunasema hapana, maelekezo
yote kuhusu Corona yanatoka kwa Mhe. Waziri Mkuu na mpaka sasa wasafiri
wanaowekwa karantini ni wanaotoka nje ya nchi,” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka ametoa wito kwa
wananchi wa mkoa wa Simiyu kufika katika vituo vya kutolea huduma za
afya na kutoa taarifa kwa wataalam wa afya pale wanapohisi kuwa na
dalili zinazotajwa kwa mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Corona ili
waweze kupata msaada stahiki wa kitaalam.
“Watu walioko karantini
hawajasakwa na polisi tunao watu wanaotoka safari za mbali na kuja
kuomba wenyewe watengwe, wengine familia zao zinaleta taarifa kuwa zina
mgeni wa aina fulani na kuomba ajitenge, jamii zetu zimekuwa na uelewa
wa kutosha kwani zinapoona mgeni zinatoa taarifa kwenye mamlaka husika
nayo inachukua hatua,”alisema Mtaka.
Katika hatua nyingine Mtaka
amesisitiza kuwa zoezi endelevu la upuliziaji dawa kwenye magari ya
abiria lifanyike mapema bila kuathiri ratiba za wasafiri huku akiwataka
makondakta kuhakikisha wanawasimia abiria wamenawa mikono yao kwa
kutumia kwa kutumia maji yenye dawa . maji tiririka na sabuni na ambao
wana vitakasa mikono wavitumie.
Mtaka amebainisha kuwa mpaka
sasa Mkoa hauna mgonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya Corona na
kuongeza kuwa ni vema wananchi watumie siku tatu kuanzia leo Aprili 17,
2020 hadi 19 Aprili, 2020 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kumuomba Mwenyezi Mungu ili
aweze kutuepusha na janga hili.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Dkt.Festo Dugange amesema hadi sasa jumla ya watu 120 kutoka nje ya
nchi wamewekwa kwenye maeneo ya uangalizi maalum (karantini) katika
mabweni ya shule za sekondari, ambapo watu 18 kati yao wameruhusiwa
baada ya kumaliza siku 14 na kugundulika kuwa hawana maambukizi ya
virusi vya ugonjwa wa homa ya mapafu (Corona COVID-19).
Kwa upande wake Kamanda wa
Mkoa wa Simiyu, Henry Mwaibambe amewataka wananchi wa Mkoa huo kufuata
maelekezo yaliyotolewa na serikali huku akiongeza kuwa jeshi hilo
halitosita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yeyote ambaye atakiuka au
kushindwa kufuata maelekezo.
Nelson Rambo ni kondakta wa
basi la Kwangus Express linalofanya safari zake Bariadi -Mwanza amesema
kuwa wanafuata maelekezo yaliyotolewa na serikali kwa abiria
wanaopandia njiani kunawa mikono pamoja na kupuliza madawa kwenye
mabasi.
Akizungumza kwa niaba ya
abiria Rehema Mapalala ameishukuru serikali kwa zoezi hilo la
upuliziaji wa madawa kwenye mabasi na kusema kuwa wamelipokea kwa furaha
kwani linajali afya za wasafiri huku akiomba elimu iendelee kutolewa
kwani siyo wananchi wote waliopata elimu ya namna ya kujikinga na virusi
vya Corona.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...