Yassir Simba, Michuzi Tv
MMILIKI na Mkurugenzi wa bendi ya muziki wa dansi nchini ya Twanga Pepeta, Asha Baraka amedai bendi yake sasa haiko sawa kiuchumi kutokana na janga la Corona.
Mkurugenzi wa bendi hiyo ameyasema hayo katika mahojiano yake na kipindi cha clouds 360 kinachorushwa na clouds TV.
Asha Baraka amedai kwamba kutokana na janga hilo la Corona kumesababishwa kufungwa kwa baadhi ya kumbi za starehe na kupelekea bendi hiyo kukosa maonyesho ambapo amedai amesaidia kuwalipa msharaha wa mwezi mmoja takribani wafanyakazi 40 wa bendi hiyo na hali ya uchumi haiko sawa kwa upande wake kupelekea baadhi ya wanamuziki wa bendi kuuza simu zao ili wajikimu kimaisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...