Kamati kitaifa ya  Makatibu Wakuu 14 ya kukabiliana na virusi vya Corona nchini imetembelea Hosteli za Magufuli katika Chuo Kikukuu cha Dar es salaam jijini humo ambako wasafiri kutoka nchi za nje wamepelekwa karantini kwa siku 14, huku wasafiri 72  wakiruhusiwa kurejea nyumbani baada ya vipimo kuonyesha hawana maambukizi ya Covid-19.

Wasafiri 226 kutoka nchi mbalimbali za nje walipelekwa karantini katika hosteli hizo na kwamba wasafiri wasafiri  72 wameruhusiwa kurejea nyumbani  na hivyo wamebaki wasafiri 154.

Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt.Rashid Mfaume wakati akitoa taarifa kwa Kamati hiyo ya kukabiliana na virusi vya Corona ambayo imetembelea Hosteli za Magufuli, Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani na kituo cha Kisoka ambacho kipo kilometa moja kutoka Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila.

Akizungumza katika ziara hiyo, Katibu wa Makatibu wakuu, Dkt. Zainab Chaula ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema Kamati hiyo imetembelea maeneo hayo ili kupata taarifa za Maendeleona mafanikio ya huduma za afya za kukabiliana na maambukizi ya  Covid-19 ambazo zinatolewa na wataalamu wa afya.

Dkt. Chaula amesema katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, jengo la kulaza wagonjwa wa Covid-19  limekamilika na kwamba wataalamu wako tayari kupokea wagonjwa wakati wowote kuanzia sasa.

“Kituo hiki au jengo hili ambalo lina vitanda 40, hivi sasa hakijapokea wagonjwa lakini wakipatikana tutawaleta hapa kwa ajili ya kuwahudumia. Pia nawashukuru Makatibu wakuu wenzangu kwa kushiriki kutembelea  vituo hivi ambavyo vimeandaliwa na Serikali kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Covid-19,” amesema Dkt. Chaula.

Katika hatua nyingine, Serikali inajenga kituo  cha kisasa cha magonjwa ya mlipuko kitakacho gharimu shilingi bilioni 7 na itakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 200 ambacho kipo eneo la Kisoka, kilometa moja kutoka Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

 Meneja Mradi wa Ujenzi wa kituo hicho Kanali Solomoni Shausi amesema kwamba mradi huo unajengwa na Suma JKT na kwamba baadhi ya majengo yatakamilika Aprili 30, mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu ya kukabiliana na COVID-19 baada ya kutembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani tarehe 8 Aprili, 2020.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu ya kukabiliana na COVID-19 na wataalamu wa Afya waliopo katika Hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam maarufu Magufuli. Kamati hiyo imefanya ziara tarehe 8 Aprili, 2020. Hosteli za Magufuli ni moja ya maeneo waliyotembelea.

Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula wakitembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, ambapo jengo moja lenye vitanda 40 litatumika kuwahudumia wagonjwa watakaobainika kuwa na virusi vya Corona.

Meneja wa mradi wa ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya magonjwa ya mlipuko, Kanali Solomoni Chausi akitoa taarifa mbele ya Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu ya kukabiliana na COVID-19 walipofanya ziara ya kutembelea mradi huo.

Meneja operesheni wa kiwanda cha kuzalisha barakoa cha kampuni ya Pristine kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam akitoa taarifa kuhusiana na kiwanda hicho mbele ya Kamati ya Kitaifa ya kukabiliana na COVID-19 walipotembelea kiwanda hicho tarehe 8 Aprili, 2020 
Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wakiwa ndani ya kiwanda cha kampuni ya Pristine kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam kuona jinsi uzalishaji wa Barakoa unavyofanyika kwenye kiwanda hicho.

Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wakiwa ndani ya kiwanda cha kampuni ya Pristine kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam kuona jinsi uzalishaji wa Barakoa unavyofanyika kwenye kiwanda hicho.

Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wakiwa ndani ya kiwanda cha kampuni ya Pristine kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam kuona jinsi uzalishaji wa Barakoa unavyofanyika kwenye kiwanda hicho.

Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wakiwa ndani ya kiwanda cha kampuni ya Pristine kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam kuona jinsi uzalishaji wa Barakoa unavyofanyika kwenye kiwanda hicho.

Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula wakitembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, ambapo jengo moja lenye vitanda 40 litatumika kuwahudumia wagonjwa watakaobainika kuwa na virusi vya Corona.

Kamati ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wakitembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, ambapo jengo moja lenye vitanda 40 litatumika kuwahudumia wagonjwa watakaobainika kuwa na virusi vya Corona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...