Kampuni ya FAMM (AMTL) ya jijini Dar es salaam, mapema wiki hii ilitembelea Kituo cha Kulelea Watoto wenye uhitaji cha Huruma kilichopo Goba, Jijini Dar rs Salaam na kuwapatia zawadi mbalimbali za Sikukuu ya Pasaka ili na wao waweze kusherekea Sikukuu hiyo, ambapo walikabidhi mahitaji mbalimbali kama mchele, mafuta, sabuni maji n.k.
Aidha, Kampuni ya FAMM (AMTL) ilipeleka vifaa mbalimbali vya kujikinga na Virusi vya Corona ikiwa ni pamoja na Sanitizer na Sabuni na mafunzo mbalimbali ya jinsi ya kujikinga na kujiweka salama na Virusi vya Corona yalitolewa kwa watoto hao.
Kwa kutambua kuwa Dunia ipo kwenye janga la Virusi vya Corona, tahadhari mbalimbali zilichukuliwa ili kuhakikiasha kila aliyeshiriki anakuwa salama ikiwa ni pamoja na Watoto wa Kituo cha Huruma.

FAMM (AMTL) ni Kampuni inayojihusisha na Uchimbaji wa Madini, Usafirishaji na Kilimo cha Biashara. Vilevile, kwa kushirikiana na Emmanuel Shija (President of World Boxing Council Muay Thai Tanzania and World Muaythai Federation Tanzania) ipo tayari kukuletea Elimu ya Michezo na kuwa Imara kuimarisha afya kwenye jamii
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...