Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Mama Queen Mlozi, amezindua ushonaji wa Barakoa (Mask) katika Chuo cha Mafunzo Ihemi cha CCM Mkoani Iringa.
Mama Queen Mlozi amefanya Uzinduzi huo leo tarehe 25 Aprili, 2020 akimuwakilisha Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally.
Katibu Mkuu wa UWT, akizundua utengenezaji huo wa Barakoa, ameeleza kuwa, "CCM imeamua kutengeneza barakoa kwa bei nafuu, kulinganisha na bei za maeneo mengine ili kutoa huduma na kuwasaidia wananchi kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona ikiwa ni jitihada za kuunga mkono mapambano ya kuutokomeza ugonjwa huo."
Ameongeza kwa kuwaomba wananchi kote nchini kununua barakoa zinazotengenezwa katika kiwanda hiko cha Ihemi, kutokana na bei nafuu ya shilingi elfu moja tu, zikizingatia ubora na viwango vinavyohitajika na mamlaka za viwango nchini.
Kwa sasa kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha barakoa takribani elfu 4000 kwa siku na uzalishaji unaongezeka kulingana na mahitaji ya wananchi.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl. Raymond Mangwala na viongozi wengine wa Chama na Serikali Mkoa wa Iringa.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Mama Queen
Mlozi, akishiriki ushonaji w Barakoa wakati wa kuzindua ushonaji wa Barakoa (Mask) katika Chuo cha Mafunzo
Ihemi cha CCM Mkoani Iringa.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Mama Queen
Mlozi, akizungumza jambo wakati wa kuzindua ushonaji wa Barakoa (Mask) katika Chuo cha Mafunzo
Ihemi cha CCM Mkoani Iringa.
Baadhi ya Mashine za kushoea Barakoa kama zionekanavyo pichani
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Mama Queen
Mlozi pamoja na Katibu
Mkuu wa UVCCM Mwl. Raymond Mangwala wakionesha barakoa zilizoshonwa
tayari kwa kutumika na Wananchi,mara baada ya kuzindua ushonaji wa
Barakoa (Mask) katika Chuo cha Mafunzo
Ihemi cha CCM Mkoani Iringa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...