Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MIAKA
saba iliyopita Waziri mkuu wa Ireland Leo Varadkar aliacha fani yake ya
udaktari na kuingia kwenye siasa na leo amerudi katika fani yake ya
awali akihudumu kama daktari ikiwa na sehemu ya kuisaidia nchi dhidi ya
mlipuko wa virusi vya Corona (Covid -19) ambapo hadi sasa taifa hilo
lina visa 4994 Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na chuo kikuu cha
Johns Hopkins siku ya Jumatatu.
Varadkar
aliyehudumu katika sekta ya afya kama daktari kwa miaka saba
aliondolewa katika usajili huo mwaka 2013 kabla ya kujisajili upya mwezi
Machi.
Mapema mwezi
Machi mwaka huu waziri wa afya nchini humo Simon Harris alieleza mkakati
wa Wizara hiyo katika Kupambana na mlipuko wa virusi hivyo na kuelekeza
ujumbe wa "Nchi yako inakuhitaji" kwa Waziri mkuu huyo.
Varadkar
atahudumia wagonjwa mara moja kwa wiki huku ikielezwa kuwa usajili wake
umelenga kuwasaidia wananchi hata kwa kiasi kidogo.
Varadkar
Leo akiwa Waziri mkuu na daktari ametokea kwenye familia ya watatibu
ambapo baba yake ni daktari na mama yake ni muuguzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...