NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
MBUNGE
wa Jimbo la Kibaha Mjini, Slyvestry Koka, amekabidhi Mizinga kumi ya
Nyuki Yenye Thamani ya Shilingi Milioni 1.5 kwa Umoja wa Wazazi(CCM)
Kibaha Mjini kwa Ajili ya Mradi wa Ufugaji wa Nyuki.
Akizungumza
Wakati wa Makabidhiano Hayo, katika Ofisi za CCM Kibaha Mjini, Jana,
Mbunge Koka Aliipongeza Jumuiya Hiyo kwa Kupata Mwenyekiti Mwenye Maono
Makubwa ya Kuiendeleza Jumuiya Hiyo kwa Kuitafutia Miradi Mbalimbali.
"Niwapongeze
Jumuiya ya Wazazi Kibaha Mjini kwa Kupata Mwenyekiti Shunda Ambaye
Anajitambua,Mbunifu na Mckarikaji katika Kutaka Kuacha Alama kwa Muda
Aliopo Madarakani katika Utawala Wake;
Aidha
Mbunge Koka, Alisema kwa Hamasa ya Maendeleo ya Jumuiya ya Wazazi
Imempelekea Yeye Kama Mwakilishi katika Jimbo Hilo la Kibaha Mjini Kutoa
Mizinga 10 Kwa Ajili ya Kuchagiza na Kutunisha Mradi wa Ufugaji wa
Nyuki Ambao Baada ya Uvunaji wa Asali Utaipatia Jumuiya Hiyo Kipato.
Akizungumza
Baada ya Kupokea Mizinga Hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Tanzania
Jumuiya ya CCM, Edwin Shunda, Alimshukuru Mbunge Koka kwa Kuipatia
Jumuiya Hiyo Mizinga 10 na Kusema Awali Walikuwa na Mizinga 30 kwa
Kuongezewa Mizinga 10 Sasa Mizinga imefika 40.
"Kwa
Niaba ya Jumuiya ya Wazazi Kibaha Mjini Tunamshukuru Mbunge Koka kwa
Kutupatia Mizinga 10 ya Nyuki Tayari Tuna Mizinga 30 Ambayo
Tumeshatundika Kwenye Shamba Letu na Hii 10 Jumla 40" Alisema Mwenyekiti
Shunda.
Pia Mwenyekiti
Shunda Alitumia Nafasi Hiyo Kuwashukuru Meneja wa Kanda wa Wakala wa
Misitu Tanzania na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti wa Miti Dawa Kutoka
Muhimbili kwa Kuipatia Jumuiya Hiyo ya Wazazi Shamba Ekari 5 na Maji kwa
Ajili ya Ufugaji wa Mradi wa Nyuki Utakaozalisha Asali Baada ya Uvunaji
na Kuiletea Fedha Jumuiya Hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...