Yassir Simba,Michuzi TV
Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouardo Philippe ametangaza rasmi kwamba ligi kuu nchini humo Maarufu kama ligue 1 matukio yote ya kimichezo kwa mwaka 2019/2020 nchini humo yamefutwa rasmi.
Uamuzi huo wakufutwa kwa matukio yote ya kimichezo nchini Ufaransa umekuja mara baada ya nchi tofauti Duniani kukumbwa na Ugonjwa wa Corona unaosababishwa na virusi vya Covid 19 ambapo mnamo tarehe 12 March mwaka huu nchi tofauti Duniani ilisimamisha shughuli zote za kimichezo katika nchi zao kutokana na ugonjwa huo.
Ufaransa sasa inakuwa nchi ya 4 Duniani kufuta shughuli zote za kimichezo mara baada ya hapo awali nchi kama Uholanzi,Ubeligiji na Argentina kutangaza kufuta matukio yote ya kimichezo katika nchi zao kutokana na ugonjwa huo wa Corona.
Kufutwa kwa ligi kuu ya mpira nchini Ufaransa itavilazimisha vilabu kama PSG na Lyon kuangalia jinsi ya kucheza michezo yao iliyobakia katika ligi ya mabingwa barani Ulaya UEFA , rasmi sasa ligi kuu imefutwa huku PSG wakiwa kinara wa ligi hiyo wakiwa na alama 68 katika michezo 27 huku klabu ya Toulause ikiwa nafasi ya mwisho ikiwa na alama 13 mara baada ya kucheza michezo 28.

Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouardo Philippe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...