Makatibu
Wakuu wa Wizara nne leo wamefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa
miundombinu ya Umwagiliaji mkoani Morogoro na kuridhishwa na kukamilika
kwa ghala la kuhifadhia mpunga kijiji cha Mvumi Wilaya ya Kilosa.
Ziara
hii imewakutanisha Makatibu wakuu wa Wizara za Kilimo Gerald
Kusaya,Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe,Naibu Katibu
Mkuu OR -TAMISEMI Bw.Gerlad Mweli na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais ,Mazingira Balozi Joseph Sokoine
Akizungumza
kwenye ukaguzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya
alisema ghala la kijiji cha Mvumi limekamilika na muda si mrefu
litakabidhiwa kwa wakulima ili litumike .
"
Wananchi wajipange kuanza kutumia ghala hili kwani kazi nzuri imefanywa
na Serikali ya Awamu ya Tano kutoa fedha nyingi kujenga mradi huu ili
usaidie kuongeza tija na thamani ya zao la mpunga kwa wakulima" alisema
Bwa.Kusaya
Mradi wa
ujenzi ghala la kijiji cha Mvumi chini ya mradi wa Kuongeza Uwezo wa
Uzalishaji wa zao la Mpunga (ERPP) umegharimu hadi sasa Shilingi milioni
735 kati ya 971 milioni utakapokamilika ambapo umefikia asilimia 99.3
Ghala
Hilo lina uwezo wa kuhifadhi tani 1300 za mpunga kwa mwaka na litakuwa
na kiwanda cha kukoboa mpunga chenye uwezo wa kukoboa kilo 1,200 kwa
siku.
Kwa upande wake
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Gerlad Mweli amewataka
wanakijiji cha Mvumi kujitolea kukamilisha ujenzi wa uzio wa ghala hilo
ili kuimarisha ulinzi.eshauri utaratibu uwekwe kwa kila mkulima
atakayetunza mazao yake ghalani kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya
ujenzi wa uzio.
Naye
mkulima James Nkalalwe wa kijiji cha Mvumi ameishukuru Serikali kwa
kukamilisha mradi huu kwani wanatarajia tija na uchumi wa wakulima
uongezeke.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof Riziki Shemdoe (aliyevaa
kofia) alikagua mtambo wa kukoboa mpunga wa katika mradi wa ghala la
kijiji cha Mvumi wilaya ya Kiliosa.Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (aliemshika bega) akitoa
maelekezo kwa mkandarasi mradiMhandisi Emanuel Norbet wa miundombinu ya
Umwagiliaji Wilaya ya Kiliosa kukabidhi mradi ifikiapo 30 Aprili
2020.Mkataba wa kazi umemalizika tarehe 21Aprili mwaka huu ambapo kazi
imefikia asilimia 84.
Ghala
la kuhifadhia mpunga kijiji cha Mvumi wilaya ya Kilosa lenye uwezo wa
kuhifadhi tani 1300 kwa mwaka likiwa limekamilika kwa asilimia 99 kwa
gharama ya shilingi milioni 735 kati ya milioni 971 chini ya mradi wa
ERPP.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...