Katibu wa Mbunge wa Singida Magharibi, Abubakari Muna (katikati), akikagua ujenzi wa nyumba ya mama na mtoto inayojengwa Kata ya Muhintiri wilayani Ikungi.
 Ujenzi ukiendelea.
 Hapa wakipeana maelekezo ya ujenzi huo.
Ujenzi wa choo cha Zahanati ya Kata ya Muhintiri ukiendelea.



Na Dotto Mwaibale, Singida.

MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu ameendelea kuunga mkono agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kuwataka wananchi kote nchini kuendelea kuchapa kazi katika kipindi hiki ambacho tunakabiliwa na ugonjwa wa corona.

Kingu licha ya kuwa Bungeni amekuwa akiendelea kutekeleza miradi yake ya maendeleo jimboni kwake kwa usimamizi wa Katibu wake Abubakari Muna jambo ambalo limewatia moyo wananchi na kujitojeza kushiriki huku wakichukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya corona.

Akizungumzia na waandishi wa habari  juzi, Kingu alisema kazi za maendeleo zinaendelea kama kawaida kama Rais John Magufuli alivyoelekeza.

"Nipo bungeni lakini kazi za maendeleo jimboni zinaendelea na zinasimamiwa na Katibu wangu Muna na wananchi wanajitokeza kwa wingi kushiriki" alisema Kingu.

Alisema miradi inayoendelea kujengwa ni ujenzi wa nyumba ya mama na mtoto na choo cha Zahanati ya Kata ya Muhintiri.

Kingu alisema mradi mwingine ni ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mpetu na Kinyampembee ambao ujenzi wake umefikia ngazi ya linta.

Rais Dkt.Johnn Magufuli alipokuwa akihutubia taifa kuhusu ugonjwa wa corona aliwataka wananchi kuendelea kufanya kazi huku wakichukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.

Alisena hakuna nradi utakaosimama kwa sababu ya kuhofia ugonjwa huo na kuwataka wananchi kila mmoja kufanya kazi ili kuinua uchumi wa nchi yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...