Mkazi wa Chanika jijini Dar es Salaam Seleman Mwamsumbwe ambaye anadai kugundua dawa ya kutibu Corona(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo akiwa nyumbani kwake kuhusu dawa hiyo ambapo ameomba kukutana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ili kuzungumza naye kwa kina. Kulia ni dada wa Mwamsumbwe Ashura Mwinyimkuu.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MKAZI wa Chanika jijini Dar es Salaam Seleman Mwamsumbwe ameomba kukutana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa lengo la kumueleza habari njema ya kwamba amegundua dawa inayoweza kutibu ugonjwa wa Covid-19 unaotokana na virusi vya Corona.

Akizungumza na waandishi wa habari leo nyumbani Chanika huku akiwa na furaha na tabasabu tele Mwamsumbwe amesema kuwa dawa hiyo ambayo ameigundua hawezi kuitaja hadharani kwa sasa hadi pale atakapoona na Waziri Ummy Mwalimu.

"Natambua changamoto kubwa Dunia inapitia kwa sasa na kusababisha mataifa mbalimbali kuhaha kutafuta tiba ya Corona. Dawa yangu ambayo tayari nimeifanyia utafiti wa kutosha nimjeridhisha ina uwezo wa kutibu ugonjwa huo bila tatizo lolote, naomba kukutana na Waziri wa Afya nizungumze naye na kisha nipate baraka ili kuokoa maisha ya watu ambayo yanaangamia kwa Corona,"amesema.

Akifafanua zaidi kuhusu dawa hiyo Mwamsumbwe amesema kwamba dawa hiyo inauwezo wa kutibu mfumo mzima wa mapafu, kuondoka mafua makali pamoja kikohozi."Namuomba Waziri wa aje tuonane ninahakika dawa hii itasaidia kuponya ugonjwa huu wa Corona au kupunguza makali ya gonjwa."amesisitiza na kuongeza anao uhakika wa asilimia 100 wa dawa hiyo kutibu Corona.

Pia amesema ameamua kujitokeza hadharani kwasababu Rais Dk.John Magufuli amonesha nia ya kuwatambua wanaotoa huduma ya tiba mbadala kuwa wanaweza kusaidia kuonesha mwanga wa kuja na dawa.

"Nampongeza Rais Dk. John Magufuli kwani ukweli ni kiongozi wa aina yake, anatambua mchango wetu na tuko tayari kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania.Ndani ya siku tatu mgonjwa anapona kabisa, nachotaka Serikali waje waiichukue hii dawa a kwenda kuifanyia kazi maabara lakini mimi sina mashaka nayo hata kidogo".

Kwa upande wake dada yake Mwamsumbwe, Ashura Mwinyimkuu amesema Serikali watakapoikubali dawa hiyo anaouhakika itakuwa msaada mkubwa kwa nchi na watu wake.

"Ombi langu Serikali iichukue hii dawa na kisha iende kuifanyia utafiti na vipimo na kisha apewe mgonjwa wa Corona, ukweli watathibitisha dawa hii kufanya kazi."amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...