Charles James, Michuzi TV

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetangaza kutumia mfumo wa malipo mtandao kwa wananchi kujaza fomu za kuomba nafasi za kufanya biashara kwenye miradi minne ya kimkakati ya Stendi ya Mabasi na Malori, Soko Kuu na eneo la Mapumziko la Chinangali.

Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema wamefanya mabadiliko hayo ikiwa ni siku mbili watangaze kuanza kutoa fomu kwa wananchi wanaotaka kuwekeza kwenye miradi hiyo.

Kunambi amesema wataalamu wa Jiji kwa kushirikiana na wale wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wa Benki Kuu wanaandaa utaratibu mzuri ambao utakamilika Jumatatu ya Wiki ijayo ili kuanza kutumika na wananchi kujaza fomu hizo.

Amesema hatua hiyo imekuja baada ya kuona mwamko wa wananchi wanaotaka kuwekeza kwenye maeneo hayo umekua mkubwa kiasi cha kusababisha mkusanyiko mkubwa jambo ambalo linahatarisha maisha kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona ambao umeshika kasi kwa sasa duniani kote.

" Tumeona mfumo wa mtandao utasaidia watu wengi kupata fomu na kuomba kuwekeza kwenye miradi hii mikubwa ya Jiji letu. Hii itakua fursa kwa wananchi wa wilaya jirani za Dodoma na mikoa mingine lakini pia hata wa nje ya Nchi kujaza fomu hizi kwa haraka zaidi.

Lakini kwa sasa pia kuna tishio la Corona na wote tunajua namna serikali yetu inavyopambana kuhakikisha wananchi wetu wanakua salama. Sasa tukaona kuruhusu wananchi waje kuchukua fomu siyo salama sana kwao kwa kipindi hiki," Amesema Kunambi.

Amewahakikishia watanzania kwamba wale wote wenye sifa za kuwekeza kwenye miradi hiyo watapata fursa na wala hakutakua na ubabaishaji wa kuwabagua watu wa kufanya biashara kwenye maeneo hayo.

" Niwatoe hofu watanzania wote serikali yao inayoongozwa na Rais Magufuli ni ya kila mwananchi hatubagui mtu yoyote. Ndio maana nimeunda kikosi kazi ambacho kitahakikisha wale wote wenye sifa wanapata nafasi na hakutakua na ubabaishaji," Amesema Kunambi.
 Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akizungumza na Wandishi wa habari leo alipokua akitangaza mfumo mpya wa kujaza fomu za kuomba kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati kwenye jiji hilo.
 Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akizungumza na Wandishi wa habari ofisini kwake leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...