Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuelezea tathmini ya hali ya Hewa kwa mwaka 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuelezea tathmini ya hali ya Hewa kwa mwaka 2019. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi akiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) moja ya picha ya utabiri leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitathmini hali ya Hewa kwa mwaka 2019.

Na Mwndishi Wetu
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema Mwaka 2019 umeweka historia ya pekee kwa kuwa wa nne kihistoria kwa kupata mvua nyingi tangu mwaka 1970. 

Akifafanua kwa baadhi ya wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi amesema nchi ilipata wastani wa milimita 1283.5 za mvua sawa na asilimia 125 ya wastani wa mvua ya muda mrefu, yaani tangu mwaka 1981 hadi mwaka 2010. 

Alisem kiwango hicho ni zaidi ya wastani wa mvua ya muda mrefu kwa milimita 256.5. huku maeneo mengi ya nchi yakipata mvua juu ya wastani katika msimu wa vuli na mvua za wastani katika msimu wa masika. 

"Kiwango cha mvua kilichorekodiwa mwezi Oktoba 2019 ni kiwango cha juu kabisa kurekodiwa tangu mwaka 1970. Wastani wa joto nchini kwa mwaka 2019 ulikuwa ni nyuzi joto 23.8 sawa na nyuzi joto 0.9, juu ya wastani wa joto wa muda mrefu (1981-2010) Kiwango hiki cha joto kimechukua nafasi ya nne katika historia ya vipimo vya joto kali tangu mwaka 1970," alieleza Dk. Kijazi.

Aidha aliongeza kuwa Miezi ya Machi na Aprili 2019 iliongoza kuwa na joto la juu ya wastani kwa nyuzi joto 1.1 (Machi) na nyuzijoto 1.6 (Aprili) ukilinganisha na wastani wa muda mrefu.

Alibainisha kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 1970 na 2019 kumekuwa na matukio kumi na matatu (13) ya mvua za za juu ya wastani katika msimu wa Vuli, na matukio manne (4) tu katika msimu wa Masika na mwaka 2003 ndio ulikuwa na upungufu zaidi wa mvua ukilinganisha na miaka mingine tangu mwaka 1970. 

"...Takwimu zinaonyesha kuwa joto la nchi limeendelea kuongezeka kwa kiwango cha juu kuanzia mwaka 1995. Ambapo joto la usiku (minimum temperature) limeongezeka zaidi ikilinganishwa na joto la mchana (maximum temperature)," alibainisha mtaalam huyo ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, WMO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...