Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed (kulia)akizungumza baada ya kupokea Msada wa Vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mchele ,Magodoro,Mashuka Taula ,Dawa za kuosha mikono Vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini na Mfanya Biashara maarufu Mohamed Raza kwa ajili ya kupambana na Maradhi ya Korona hafla iliofanyika nje ya ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil Kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini na Mfanya Biashara maarufu Mohamed Raza kwa njia ya kugongana Miguu katika hafla ya upokeaji Msaada wa Vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mwakilishi huyo kwa ajili ya kupambana na Maradhi ya Korona iliofanyika nje ya ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil Kikwajuni Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...