Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MCHORAJI
na mwongozaji wa vibonzo vya panya (Tom) na paka (Jerry) Eugene Merrill
Deitch amefariki dunia ghafla akiwa na umri wa miaka 95 huko nyumbani
kwake Prague, mchapishaji wake Peter Himmel ameieleza The Associated
Press.
Imeelezwa kuwa
Eugene aliyezoeleka kuitwa Gene ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Oscar
alifariki dunia ghafla siku ya Alhamisi usiku akiwa katika makazi yake.
Gene
ameongoza sehemu zipatazo kumi na tatu za vibonzo vipendavyo na watoto
ulimwenguni kote maarufu kama "Tom and Jerry" pamoja na baadhi kutoka
mfululizo wa visa vya Popeye.
Gene
aliwahi kufanya kazi kama msanifu wa anga la Amerika Kaskazini kabla ya
kuandikishwa jeshini na kuingia katika mafunzo ya majaribio ya urubani
na mwaka 1959 alihamia katika makazi yake huko Prague.
Aidha
filamu yake ya Munro ilishinda tuzo filamu bora ya picha na michoro
mwaka 1960 na alichaguliwa mara mbili katika uteuzi wa kipengele cha
namna hiyo mwaka 1964 kwa filamu za Nudnik na How to Avoid Friendship.
Awali Gene alitengeneza mfululizo wa filamu ya visa ya Tom ambapo Sidney's Family Tree iliteuliwa katika tuzo Academy mwaka 1958.
Gene alikua akiishi na mkewe na watoto wake wa kiume watatu kutoka ndoa yake ya kwanza ambao wote ni wahusika katika vibonzo.
Mashibiki
wengi wameeleza kusikitishwa na kifo hicho ambapo kurasa nyingi za
Twitter zimejaa Salamu za rambirambi kufuatia kifo hicho ambapo wengi
wameeleza kuwa Gene alikuwa zaidi ya Tom na Jerry na atakumbukwa daima
kupitia vibonzo hivyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...