NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ametoa pole kwa familia 21 zilizopata msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani na kuwataka wananchi kuchukua taadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Akizungumza na wanafamilia hao aliowatembelea kuwapa pole katika kata saba za Wilaya ya Mkuranga, Ulega aliwapatia kiasi zaidi ya Sh.milioni moja na unga kwa familia hizo za marahemu.
Aidha Ulega amesema amesikitishwa na msiba huo na kuwataka wafiwa wote kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu. "Nchi yetu hipo katika janga la corona kwahiyo tuchukue tadhari Kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na serikali."
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga Juma Athuman Abeid amesema watafatilia ili kuhakukisha watu wote waliopata ajali wanapata haki zao kupitia bima.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi mbunge wa Mkuranga mkoa Pwani Abdallah Ulega (wapili kulia) akiwa ameambatana na ziongozi mblimbli wa wilaya hiyo wakielekea kata ya Magawa kuwapa pole wanafamilia waliopatwa na msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani.Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega (kulia)akiwapa pole wanafamilia waliopatwa na msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani,(katikati) ni Mwenyekiti wa halmashaul ya Wilaya Mkuranga na Diwani wa kata ya Magawa,Juma Abed
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega (kushoto)akiwapa pole wanafamilia waliopatwa na msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani,ambapo aliwaomba wananchi kuchukua taadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Mwenyekiti wa halmashaul ya Wilaya Mkuranga na Diwani wa kata ya Magawa,Juma Abed (alievaa kanzu) akiwapa pole wanafamilia waliopatwa na msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani,ambapo amesema watafatilia ili kuhakukisha watu wote waliopata ajali wanapata haki zao kupitia bima.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega ametoa pole kwa familia 21 zilizopata msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani.(Picha zote na Emmanuel Massaka,Michuzi Tv)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...