Na
Amiri kilagalila,Njombe
HALMASHAURI ya wilaya ya Njombe ambayo asilimia 70 ya mapato yake inayapata
kutoka kwenye mazao ya miti , imefanikiwa kuvuka tena lengo la makusanyo ya
mwaka 2019/2020 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka kwa kukusanya asilimia
108 ya mapato.
Ripoti hiyo ya makusanyo imetolewa katika kikao cha baraza na mwenyekiti wa
halmashauri Valentino Hongoli na kutolewa ufafanunuzi na mkurugenzi Ally Juma
ambaye anasema siri ya mafanikio makubwa katika makusanyo yametokana na
ongezeko la udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato,Matumizi ya mashine za POS
pamoja na kuweka mageti zaidi ya 18 ya ukaguzi na kwamba matarajio ni kukusanya
zaidi siku za usoni.
“Upande
wa mapato ya ndani pekee halmashauri ilikisia kukusanya kiasi cha shilingi
bilioni 1.8 kutoka vyanzo vya ndani,lakini hadi kufikia mwezi machi 2020
halmashauri imefanikiwa kukusanya kiasi cha bilioni 1.9 sawa na 108% hii
inamaanisha halmashauri imefanikiwa tena kuvuka malengo”alisema Valentino
Hongoli
Jitihada kubwa za makusanyo ambazo zinatajwa kuchangiwa na uzalishaji mkubwa wa mbao,viazi na mahindi unamsukuma mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri wakati akitoa salamu za serikali ambapo ameitaka halmashauri hiyo kuanzisha kiwanda cha kuzalisha samani ili kunufaika zaidi na mazao ya misitu badala ya kuuza miti na mbao tu.
“Tunasafirisha mbao nyingi,lakini tunapata hela kidogo sana katika mapato hebu tubadilishe sasa tusafirishe lakini tutengeneze wenyewe,tutainua vijana wajasiriamali ambao tutawjengea kitu kikubwa na itakuwa ni ajira kwao”alisema Ruth Msafiri
Wakibainisha sababu zilizokuwa zikichangia kuwa na upotevu mkubwa wa mapato katika halmashauri hiyo baadhi ya madiwani akiwemo Roida Wanderage na Shaibu Masasi wanasema kipindi cha nyuma kulikuwa na utoroshaji wa mapato na wizi wa fedha za ushuru jambo ambalo limedhibitiwa vyema na matumizi ya mashine za POS.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli wakati akitoa taarifa ya
halmashauri na kufungua kikao cha baraza la madiwani.Jitihada kubwa za makusanyo ambazo zinatajwa kuchangiwa na uzalishaji mkubwa wa mbao,viazi na mahindi unamsukuma mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri wakati akitoa salamu za serikali ambapo ameitaka halmashauri hiyo kuanzisha kiwanda cha kuzalisha samani ili kunufaika zaidi na mazao ya misitu badala ya kuuza miti na mbao tu.
“Tunasafirisha mbao nyingi,lakini tunapata hela kidogo sana katika mapato hebu tubadilishe sasa tusafirishe lakini tutengeneze wenyewe,tutainua vijana wajasiriamali ambao tutawjengea kitu kikubwa na itakuwa ni ajira kwao”alisema Ruth Msafiri
Wakibainisha sababu zilizokuwa zikichangia kuwa na upotevu mkubwa wa mapato katika halmashauri hiyo baadhi ya madiwani akiwemo Roida Wanderage na Shaibu Masasi wanasema kipindi cha nyuma kulikuwa na utoroshaji wa mapato na wizi wa fedha za ushuru jambo ambalo limedhibitiwa vyema na matumizi ya mashine za POS.
Baadhi
ya viongozi wakati wakisikiliza hoja za madiwani wakati wa kikao cha baraza la
madiwani halmashauri ya mji wa Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...