
WAKATI idadi ya wagonjwa wa Covid-19 nchini ikifikia 147, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imetangaza kupiga marufuku mikusanyiko ya watu kwenye baa zote ndani ya wilaya hiyo na kwamba wanywaji watalazimika kununua vinywaji na kwenda kunywea majumbani.
Marufuku hiyo imetangazwa leo Aprili 17 mwaka huu wa 2020 ,hivyo wamiliki na wahudumu wote wa baa wanatakiwa kufuata maelekezo hayo ambayo ni moja ya mkakati wa Kupambana na virusi vya Corona.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari, amesema uamuzi huo unalenga kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo huku akisisitiza kuwa waendesha baa hizo, kuuza vinywaji hivyo lakini lakini mnunuzi lazima akanywee nyumbani."Atakayekaidi agizo hili atachukuliwa hatua".
Mjema amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kuzingatia maelekezo hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mwendeshaji wa baa na mtu yeyote atakayeonekana kwenye eneo la baa akiendelea kunywa wakati agizo hilo limeshatolewa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...