Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
POLISI
mmoja nchini India amekatwa mkono kwa upanga na maafisa wengine sita
kujeruhiwa vibaya mara baada ya kushambuliwa wakati wa kutekeleza zuio
la watu kutoka nje (Lockdown) ikiwa ni sehemu ya kuzuia kuenea kwa
virusi vya Corona (Covid -19) huko Punjab kaskazini mapema leo asubuhi,
Shirika la kimataifa la utangazaji la CNN limeripoti.
Imeelezwa
kuwa sehemu ya mkono (kiwiko) wa kushoto wa Harjit Singh, mkurugenzi
msaidizi wa Polisi wa Punjab ulijeruhiwa vibaya na baadaye ilirudishiwa
kwa kufanyiwa upasuaji uliodumu takribani masaa nane.
Shambulio
hilo lilitokea wakati gari lililokuwa limebeba watu saba waliosadikika
kuwa ni wanakikundi cha wapiganaji wachache wa Sikh kinachojulikana
kama Nihangs waliosimama katika uwanja wa biashara nje ya soko la mboga
wilayani Patiala na polisi walipowauliza wanaume hao hati halali za
kusafiri, mmoja wao akatoa upanga kumkata mkono Singh.
Aidha maafisa wa polisi wameonesha silaha zenye ncha kali zilizopatikana huko Patiala, India, Aprili 12.
Maafisa
wengine waliojeruhiwa, mmoja akiwa na majeraha ya upanga mgongoni
walipelekwa katika Taasisi ya Uzamili ya Mafunzo ya Utabibu na Utafiti
huko Chandigarh.
Kiongozi
wa Serikali nchini humo Amarinder Singh kupitia ukurasa wake wa
Twitter amechapisha taarifa inavyoeleza namna upasuaji wa kurudisha
sehemu ya mkono (kiwiko) ulivyochukua takribani masaa manane na
amewashukuru madaktari na wafanyakazi kwa msaada na kumtakia Harjeet
Singh ahueni ya haraka.
Aidha imeelezwa kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote ambaye atakiuka taratibu na muda uliopangwa.
Kufuatia
operesheni ya saa moja katika gurdwara ya eneo hilo (hekalu la Sikh)
polisi waliwakamata watu hao saba waliotuhumiwa na uchunguzi zaidi
unaendelea.
Kwa mara ya kwanza India imefunga reli zake katika miaka 167 na sasa treni zimegeuzwa kuwa hospitali.
India
kwa sasa iko chini ya kizuizi cha kitaifa hadi Aprili 30 huku Punjab
likiwa jimbo lililoripoti jumla ya kesi 151 zilizothibitishwa za virusi
vya Corona, wagonjwa waliopona 5 pamoja na vifo 11.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...