NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amepokea vifaa vya Kunawia
Mikono ,tenki 25 za maji kutoka Kampuni ya Motisun Group vyenye thamani
ya Sh.6.2 ikiwa ni jitihada za Mkoa kushirikiana na Wadau katika
mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Ndikilo
ametumia pia,wasaa huo kuwakumbusha na kuwaonya baadhi ya abiria
wanaokaidi agizo la kuvaa barakoa ambalo wataalamu wa afya wamekuwa
wakielekeza ili kupunguza maaambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.
Akizungumza
wakati wa upokeaji wa vifaa hivyo ,alisema vifaa hivyo vitagawanywa
katika Hospitali ya Mkoa na za Wilaya, Kituo cha Matibabu ya Covid 19
Lulanzi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Ofisi za
Wakurugenzi wa Halmashauri ,Masoko,Kituo Cha Afya Mkoani, Mlandizi ,Kibiti, pamoja na Shirika la Nyumbu .
"
Wananchi tuvae barakoa na kuzingatia level sit kwenye vyombo vya safari
hii ni kwa afya zetu hata mkisimama si kwa hasara ya mtu mwingine ni
wewe na familia yako" alisema Ndikilo.
Ndikilo
alielekeza wahusika katika Mkoa huo kufuatilia suala hilo kwani kwa
kuendelea kuwaacha baadhi ya watu wakisafiri bila kuvaa barakoa ni Moja
ya Maeneo ambayo yana uwezekano wa kuambukizana.
Aidha, alisema kwa sasa wazazi watunze watoto wao wasizurure mtaani kwa hali ilivyo ambayo ni hatari.
Hata hivyo, Ndikilo aliwakumbusha wazazi kuwa Serikali imefunga Shule hivyo amewataka kuzuia watoto wao kuzurura Mitaani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...