Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo akipimwa hali yake ya joto la mwili kabla ya kuingia katika
ofisi za kituo cha Uhami`aji kilichopo katika mpaka wa Kasesya
unaotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia,uliopo kata ya Itete, Wilayani
Kalambo.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo akitoa maelekezo kwa maafisa wa uhamiaji pamoja na watumishi wa
mpaka wa Kasesya unaotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia kuhakikisha
wananchi wanaotumia mpaka huo wanazingatia usafi.

Afisa Afya wa Wilaya ya kalambo
Richard Manuma (Kulia) akitoa maelezo juu ya maandalizia ya hema
linalotumika kwaajili ya kuwaweka Karantini siku 14 wasafiri wanaotumia
mpaka wa Kasesya unaotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia katika Wilaya
ya Kalambo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
(kushoto).

Mkuu wa mkoa wa Rukwa na kamati
yake ya Ulinzi na Usalama wakitoka katika geti (nyuma yao)
linalotenganisha mpaka wa Tanzania na Zambia baada ya kutembelea mpaka
huo na kujiridhisha juu ya udhibiti wa utumiaji wa mpaka huo kwa
watanzania na wazambia.
……………………………………………………………………………………………….
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameitaka Kamati ya maafa ya Mkoa kuhakikisha
wanaendelea kutoa elimu kuanzia ngazi ya Kijiji, Mtaa, Kata, Tarafa hadi
Mkoa huku akisisitiza mkazo wa kutolewa kwa elimu hiyo uelekezwe kwa
vijana ambao wengi wao wanaonekana kutofuatilia taarifa za habari pamoja
na elimu mbalimbali zinazotolewa na vyombo vya habari juu ya ugonjwa wa
Corona.
Amesema kuwa
vijana wa kisasa kuanzia mjini mapaka vijijini wamekuwa wagumu
kusikiliza taarifa ya habari kwenye redio wala kuangalia taarifa ya
habari kwenye runinga zaidi ya kujiendekeza kusikiliza muziki bila ya
kujali na kutaka kujua serikali inasema nini juu ya kujikinga na maradhi
hayo ya Corona.
“Akitembea kuna
vitu viko masikioni humu anasikiliza muziki tu, nini serikali inasema
kuhusu janga hili hajui, lakini mambo haya yanazungumwa sana kwenye
redio, yanasemwa sana kwenye televisheni zetu, program ziko nyingi
lakini vijana na kundi kubwa wanaonekana hawana muda wa kufuatilia,
tuwarudishe hili kundi kubwa, lijenge tabia ya kufuatilia nini
kinazungumzwa kwenye redio, kila redio inazungumza, ziko redio za ndani
ziko redio zenye sura ya kitaifa,” Alisisitiza.
Aliongeza kuwa
hii inaweza kuwa vita ya tatu ya dunia isipokuwa adui hatumuoni hivyo
hatuna budi kila mmoja kwa nafasi yake akaendeleza kutoa elimu bila ya
kuchoka ili kuweza kupambana na adui huyu ambaye haijulikani lini
atashindwa.
Ameyaongea hayo
wakati alipofanya kikao na kamati ya maafa ya mkoa iliyowajumuisha
waganga wakuu wa wilaya wakiongozwa na mganga mkuu wa mkoa, viongozi wa
dini na wataalamu wa ustawi wa jamii pamoja na maendeleo ya jamii wa
mkoa na taasisi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na kutoa elimu za
afya katika mkoa.
Aidha,
Alisisitiza ili kuweza kufanikisha kufikisha elimu kwa wananchi wote wa
mkoa huo hakuna budi kuwaelimisha viongozi wa ngazi zote wakiwemo
wenyeviti wote wa vijiji na mitaa ili watilie mkazo utekelezaji wa
maelekezo ya serikali katika maeneo yao ya kiutawala.
Kuhusu ulinzi wa
Mipakani Mh. Wangabo alisema kuwa Mkoa wa Rukwa una vipengo 50 katika
ziwa Tanyanyika ambavyo hutumika na wananchi wan hi ya jirani ya Kongo
na hivyo kuwataka wananchi kuwa makini na wavuvi wote wanaotoka katika
nchi hiyo kuhakikisha wanawarudisha walikotoka na kisha kuripoti kwa
vyombo vya usalama na kusisitiza kuwa wananchi wa maeneo hayo wanapaswa
kuwa walinzi wa kwanza wa usalama wa nchi yetu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...