NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
MBUNGE
wa Jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amekabidhi mabati 1,000 kwa
halmashauri ya Chalinze ,pamoja na tanki za maji na mabeseni Tisa vyote
vikiwa na gharama ya milioni 13.9.
Kati
ya mabati hayo 600 yataelekezwa katika miradi ya halmashauri ya sekta
ya elimu na afya na 400 yatapangiwa kazi na matakwa ya mfuko wa jimbo.
Akizungumzia
kuhusu msaada huo ,Ridhiwani alieleza kuwa , shule ya sekondari
Changarikwa inapatiwa mabati 90,Msata 90,Chamakweza mabati 90,nyumba ya
mwalimu sekondari ya Lugoba mabati 30 na shule ya msingi Magome mabati
60, Msolwa 60,Kidogozero mabati 90 na Ruvu Darajani.
Alisema,matanki ya maji yanakwenda katika vituo vya afya,zahanati ili kujikinga na janga la ugonjwa wa corona.
Ridhiwani
alieleza ,kwasasa jamii inapaswa kujihadhali na ugonjwa huo hivyo
akaona umuhimu wa kutafuta mdau Shubash Patel ambae alitoa matanki tisa
aina ya Kiboko pamoja na mabati kwa ajili ya kuezeka miradi ya afya na
elimu jimboni hapo .
"Kuna
maeneo ya mkusanyiko mahitaji bado ni makubwa ya ndoo za maji kwaajili
ya wananchi kunawa maji ,kama pale mnada wa Bwilingu ,nilitembelea wiki
iliyopita mahitaji ni makubwa " alisema Ridhiwani.
Kutokana
na hilo pia amempata mdau mwingine ambae atamsaidia kuleta ndoo 30 kwa
ajili ya kulinda na corona pamoja na makopo ya rangi na gymsum:;anasema
Ridhiwani.
Nae
mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze, Amina Kiwanuka alimshukuru
mbunge wa Chalinze kwa ushirikiano anaouonyesha katika kutatua
changamoto za kimaendeleo .
Kwa
upande wake ,meneja uajiri wa Kampuni ya Sayona ,Godlove Mngwamba
alisema mbunge Ridhiwani alipeleka maombi ofisini kwao na kutokana na
utekelezaji na uwajibikaji wake katika kuwatumikia wananchi wamekubali
kusaidiana nae kutatua changamoto mbalimbali kwa jamii.
Alisema ,hawatasita kuwa karibu na jamii kwakuwa ni muwekezaji mkubwa na anapaswa kushirikiana na jamii .
Godlove
alifafanua ,ugonjwa wa corona ni janga la kupambana nalo hivyo wametoa
matanki ya maji na mabeseni kwa ajili ya kutumika kwenye zahanati na
vituo vya afya.
Alisema ,kuhusu mabati wametoa mabati 1,000 vitu vyote vikiwa na gharama ya milioni 13.9.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...