KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP)Blasius Chatanda akiwaonyesha waandishi wa habari vitu ambavyo
vimekamatwa wakati wa opeseheni hiyo.
Camera ambazo pia zimekatwa wakati wa operesheni hiyo.


KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP)
Blasius Chatanda akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali

 
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP)
Blasius Chatanda ametoa onyo kali kwa wezi wanaovunja nyumba za watu na
kuiba mali kwa kuwataka waache mara moja tabia hiyo kabla
hawajafinyangwa finyangwa.

Chatanda aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba awali kulikuwa kumeibuka wimbi la uvunjaji wa nyumba hali ambayo iliwalazimu kuanzisha operesheni kabambe ya kuwasaka ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani.

Alisema kwamba katika operesheni hiyo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 8 ambao kwa sasa wapo mahabusu ambapo walikamatwa wakiwa na vitu mbalimbali ambavyo waliviiba kwenye maeneo mbalimbali  Jijini Tanga.

Kamanda Chatanda alitaja vitu ambavyo vilikamatwa kuwa ni TV Flat Screen 7zenye ukubwa wa tofauti kuanzia nch 50 hadi 21 ambazo zinadaiwa ziliibiwa kwenye baadhi nyumba za kulala wageni zilizopo Jijini Tanga.

Aidha alisema pia katika operesheni hiyo waliwakamata vitu vingine ikiwemo Kompyuta mpakato  16,simu za mkononi 7 ambapo baadhi ya vitu hivyo viliibiwa kwenye nyumba
za kulala wageni.

“Tunaomba walioibiwa waje watambue mali zao kama ni miongoni mwa zilizokamatwa huku akisisitiza kwamba msako huo ni endelevu na hakuna mtu ambaye hatabaki salama “Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga.

Kamanda huyo alisema kwamba msako huo ni endelevu na
hakuna mtu ambaye atabaki salama huku akieleza kwamba kwa waliozoea
kuiba watafute kazi nyengine za kufanya kwa sababu wakikamatwa
watawafinyangwafinyanwga mpaka wasahau njia walizokujia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...